washabiki wa timu ya AJTC wakiwa wanashangilia mara baada yakukabidhiwa kombe katika bonanza la Taswa
mwenyekiti wa Taswa Taifa Juma Pinto akiwa akiwa anakagua timu ya mpira wa pete kutoka AJTC kabla ya mechi ya fainaili kuchezwa
Meneja masoko wa Mega trade, Godluck Kway akitoa neno ndani ya bonanza hilo
Mkuu wa matukio ya kanda ya kaskazini Bw. Christ Sarakana kutoka TBL akiongozana na meneja masoko na mauzo wa kampuni ya Mega Trade Investment Godluck Kway kukagua timu ya netball ya chuo cha uandishi wa habari AJTC
kikosi cha timu ya mpira wa miguu kutoka cho cha AJTC
Nahodha wa timu ya mpira wa miguu wa AJTC Bw. Alli Ahmedi akikabidhiwa kombe la ubingwa na Mkuu wa matukio ya kanda ya kaskazini Bw. Christ Sarakana kutoka TBL
Timu za Chuo Cha Uandishi wa Habari Arusha (AJTC) juzi zilitwaa ubingwa katika bonanza la tisa la waandishi wa habari Kanda ya Kaskazini, lililofanyika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Katika bonanza hilo, ambalo mgeni rasmi alikuwa, Mwenyekiti wa Taswa Taifa, Juma Pinto jumla ya timu 10 zilishiriki na liliandaliwa na Taswa Arusha kwa ushirikiano na kampuni ya Ms Unique.
Timu ya soka ya AJTC ilitwaa ubingwa baada ya kuifunga kwa mikwaju ya penati 5-4 timu ya Radio Sunrise, wakati wasichana wa timu hiyo, waliwashinda timu ya chuo cha uandishi wa habari na maendeleo ya jamii (IMS), magoli 18-5.
Mgeni rasmi Pinto ambaye pia ni Mjumbe wa bodi vya Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro alikabidhi vikombe na fedha taslimu, ambapo bingwa wa soka alipewa kikombe, pamoja na fedha taslimu 200,000 na seti ya jezi.
Mshindi wa pili wa soka akipata 100, 000 wakati bingwa wa mpira wa pete alizawadiwa kikombe na fedha taslimu 100, 000 huku mshindi wa pili akikabidhiwa tsh 50, 000.
Katika bonanza hilo, ambalo lilidhaminiwa na kampuni ya bia nchini, (TBL), kampuni ya Megatrade Investment, Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro, Cocacola, SBC (T) ltd, AICC, Tanzanite Forever, TANAPA na Alphatel,
Timu zilizoshiriki ni Radio 5, timu ya Arusha One, ORS kutoka mkoa wa Manyara, Salam Club, IMS na Taswa Arusha ambayo iliibuka na ushindi katika kukamata kuku.
Akizungumza katika bonanza hilo, Pinto alipongeza washindi na viongozi wa Taswa Arusha kwa kazi nzuri waliofanya.
“Nachukuwa fursa hii kuwapongeza sana Taswa Arusha kwa kuandaa bonanza hili kwani halifanyiki sehemu nyingine nchini”alisema
Awali Meneja matukio wa TBl, Chris Sarakana aliahidi TBL kuendelea kudhamini bonanza hilo kutokana na kuvutia wanahabari na wakazi wengi wa Arusha.
Meneja masoko wa Mega trade, Godluck Kway aliwapongeza wanahabari kwa kushiriki kwa wingi katika bonanza hilo na kuahidi kuendelea kulidhamini.
CHANZO: LIBENEKE LA KASKAZINI
0 maoni:
Post a Comment