Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mgambo wa Jiji Arusha Wanakosa Busara ya Kutekeleza Majukumu Yao Bila Kukwaruzana na Wanajamii

Blog hii ilikutana na tukio hili jana jioni katika pitapita yake katikati ya  mitaa fulani ya Jiji la Arusha. Mgambo wa Jiji wakilazimisha kuondoka na machungwa ya kijana anayeonekana pichani, aliyekataa kuiba na kuamua kujikusanyia sh mia mia halali. Wote majina yao hayakuweza kupatikana haraka.

Pamoja na sheria za kutoruhusu biashara kienyeji mijini, utekelezaji wake ni wa hovyo na kudhalilisha sana, hususani kwa Jiji letu la Arusha. Mgambo wa Jiji wamekuwa wakatili kiasi cha kukosa busara ya kutekeleza majukumu yao bila kukwaruzana na jamii husika.

Kwa mfano, kama nia ni kuwa na mgambo wanaozurura muda wote ili mtu asiweze kufanya biashara pasiporuhusiwa maana yake ni kwamba yeyote akionekana anajaribu anzuiwa.

Sasa ajabu hawa 'law enforcers' wao hawana habari na kwamba wamefanikiwa kumzuia mtu, bali kwao ni lazima wapore na mali zake..mbaya zaidi kama ni za kuliwa wazile. Nikajiuliza hivi siku mtu akaamua kuwategeshea sumu na uroho wao watapona!??

Purukushani ya kupora machungwa yaliyokuwa kwenye ndoo ya kijana huyo anatembea nayo iliishia kujaza umati wa watu na vurugu bila sababu ambapo wangeweza tu kumwamuru aondoke mahala hapo na hata kumuelekeza katazo husika. Baadae machungwa yale yalichukuliwa na raia mmoja aliyeingilia kati na kwenda kuyahifhadhi mahali kwa vile ndio yalikuwa kiini cha mvutano, huku kijana akiwa amepandwa na hasira na mgambo hao nao wakitaka kuonesha nafasi yao.

IMG-20140702-WA0011Hii inatukumbusha pia kukosa weledi kwa baadhi ya askari Polisi wanaokwenda kutawanya kundi la watu mahala fulani na badala yake wanalazimisha kuvunja miguu hata waliotawanyika. Kwamba unakuta amri ya kutawanyika imetolewa na haijatekelezwa. Lengo la amri ni kuwataka watawanyike eneo fulani. Sasa nguvu inaweza kutumika kuwatawanya pengine kwa kupiga mabomu ya kutoa machozi.

Ajabu sasa, wakati watu wale wanakimbia huku na huko kutawanyika kinguvu, unamuona askari anamuandama mtu mmoja tuu hata kama ataingia ndani umbali gani yeye yuko nae, atamkata ngwala, atadondoka chini na kuanza kumvunja miguu na marungu. Unajiuliza hivi lengo ni kuwataka watawanyike ama ni kuwaumiza? Sasa mbona wanamuandama mtu ambaye ameshondoka eneo la tukio?

Wenyewe watakwambia lazima wapate sample za watu wa kushitaki. Lakini hatari yake ni kwamba huishia kukamata hata wasio husika na pengine kuwatia ulemavu bila hatia.

Nadhani jambo la muhimu kwa migambo hawa na askari wengine ni kutimiza wajibu wao kwa kuwatendea binadamu wenzao yaliyohaki huku busara ikitawala zaidi. Kinyume na hapo ni kutengeneza uadui baina yao na jamii!

Washirikishe Google Plus

About Ujenzi Connekt

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO