Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA: MAPOKEZI YA DIAMOND PLATNUMZ AKITOKEA MAREKANI KATIKA TUZO ZA BET

Tarehe 10/7/2014 ni siku ambayo Star wa muziki wa Bongo fleva nchini Tanzania Diamond Platnumz, ambaye anachafua anga la muziki kwa sasa kwa utunzi na uimbaji wake alitua katika Uwanja wa Ndege Mwal. Jurius Nyerere, mnamo mishare ya saa nne na nusu za usiku akitokea nchini Marekani ambapo alikua huko kushiriki katika Tuzo kubwa Dunia  BET awards, ambazo hufanyika kila mwaka, Diamond alikua katika kategori ya Best African Act ambayo ilichukuliwa na Davido kutoka Nigeria.

Watanzania wenye moyo wa Upendo na Kizalendo walijitokeza katika viwanja vya ndege kumpokea Msanii huyo, wakiwa na mabango makubwa kabisa yenye maneno ya kuashiria ushujaa aliouonyesha Diamond katika muziki na kuipeperusha vyema  Bendera ya Tanzania katika muziki, Uwanja wa ndege wa Mwl. Julius Nyerere, uligubikwa na Kelele za Furaha na Sauti zilisikika zikiimba wimbo wa Mdogomdogo ikiwa ni mapenzi ya dhati kabisa kwa Diamond kwa kutuwakilisha vema na kurejea salama, hakika kazi ya muziki wetu kwa sasa inaonekana.

Diamond baada ya kufika aliwashukuru wote waliofika kumpokea na kusema kuwa safari yake ilikua nzuri na amejifunza vitu vingi sana pia amekutana na watu wengi na tutaraji mengine mengi na mazuri katika muziki wetu, na kwa upande mwingine alitoa shukran za dhati kabisa kwa watanzania kuipokea vema video yake mpya ya mdogomdogo, imekua ikifanya vizuri sana na hata youtube imekuwa na views wengi kwa muda mchache

























PICHA KWA HISANI YA VIJANA NA MATUKIO

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO