Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mamlaka ya Mawasiliano, TCRA yapata cheti cha Kimataifa

tcra2MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetakiwa kuongeza juhudi katika kuboresha sekta hiyo, baada ya kukabidhiwa cheti cha kiwango cha kimataifa na Shirika la Viwango Duniani.

Cheti hicho kilikabidhiwa jijini Dar es Salaam jana, mbele ya wafanyakazi wa TCRA na Mkaguzi wa kimataifa kutoka Uingereza, Andrew Rowe na kumkabidhi Mkurugenzi wa TCRA, Profesa John Mkoma.

Akipokea cheti hicho, Profesa Nkoma, alisema wamepata cheti hicho kutokana na utendaji kazi wa mamlaka hiyo katika kudhibiti mawasiliano nchini.

Alisema umefikia wakati wa sekta hiyo kufanya kazi kwa ufanisi ili ifikapo mwaka 2017, shirika hilo litakapokuja kufanya ukaguzi wakute utendaji kazi upo juu zaidi.

“Cheti tulichopata ni ISO 900:2008, kimetokana na ushirikiano tulionao miongoni mwa wafanyakazi wote na sio mkurugenzi peke yake, tutaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kutetea cheti hiki ambacho kinadumu hadi mwaka 2017,” alisema Prof. Mkoma.

Rowe aliitaka TCRA kuhakikisha wanapigania katika utoaji wa huduma bora, ili kuendelea kubaki na cheti hicho kinachowatambulisha kimataifa.

CHANZO: TANZANIA DAIMA

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO