Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Sinema la Mchana: Polisi Arusha Waua Watatu Wanaodhaniwa Kuwa Majambazi Waliokuwa Wamejipanga Kupora Mamilioni ya Fedha

JESHI la polisi mkoani hapa limewaua majambazi watatu waliokuwa wamepanga njama ya kwenda kupora mamilioni ya fedha zilizokuwa zinapelekwa benki na kampuni ya Arusha Islamic Centre inayohusika na utengenezaji na uuzaji wa vigae iliyopo eneo la Esso  mjini hapa.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa polisi mkoani hapa, Liberatus Sabas alisema kuwa,majambazi hao watatu  waliuawa jana tarehe 3 eneo la TBL –Njiro  wakiwa kwenye harakati za kwenda kupora fedha hizo.
Alisema kuwa, majambazi hao walikuwa mahali wanapanga njama majira ya saa 4;20 asubuhi wakisubiria kuteka gari lililokuwa limebeba  fedha zilizokuwa zinapelekwa benki zaidi ya milioni 100  huku wakiwa na gari aina ya Toyota Corola yenye namba za usajili T 762 CWE.
Alisema kuwa, raia wema walitoa taarifa kuhusiana na tukio hilo ndipo  polisi walifika eneo ambalo majambazi hao walikuwa wamejificha katika  eneo la unga ltd relini ambapo majambazi hao walishtuka na kuanza kuirishia gari hiyo ya polisi risasi.

Ambapo majibizano yalianza kati ya majambazi hao na polisi huku wakirushiana risasi hadi eneo la TBL njiro ndipo majambazi walipofika eneo hilo waliamua kutelekeza gari na  kushuka chini  na kumimina risasi kwa askari polisi  hao.
Kamanda Sabas alisema kuwa,hatimaye polisi waliweza kuwauawa majambazi hao  na kufanikiwa kuchukua silaha yao aina ya shortgun yenye namba A 947514 M aina ya  Pumpaction ikiwa na risasi 3 .
Kamanda alisema kuwa, bado majina ya majambazi hayo hayajafahamika ambapo wanakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 hadi 30 na miili yao imehifadhiwa katika hospitali ya mkoa ya mount Meru.
Aidha Kamanda aliwashukuru wananchi kwa juhudi kubwa sana walizoonyesha na ushirikiano hadi kukamatwa kwa majambazi hayo na kuwataka kuendelea kuongeza juhudi hizo zaidi.

 

STORI: LIBENEKE LA KASKAZINI

PICHA:  SERIA

Gari iliyokuwa na majambazi hayo baada ya kushamuliwa kwa risasi na mmoja kuuawa.

Jambazi mmojawapo aliyeuawa kwa kupigwa risasi akiwa ndani ya gari

Jambazi mwingine aliyeuawa eneo la jirani ba Baclays Bank jijini Arusha

Askari wakilikagua gari hilo.

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO