Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Hatariiii! Mabomu Tena Arusha: Mgahawa wa Kihindi Walipuliwa na Bomu; 8 Wajeruhiwa Vibaya

Mlipuko unaosadikiwa ni bomu umelipuka usiku wa kuamkia leo jijini Arusha  katika mgahawa wa  Traditional Indian Cusine uliopo pembezoni mwa hotel ya Gymkana jijini hapa na kujeruhi watu nane

Akithibitisha kupokea wagonjwa walioadhiriwa na bomu hilo  Mkurugenzi wa tiba ambaye pia ni kaimu mgamg a mkuu wa hospitali ya Selian, Dr Paulo Kisanga alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 4:30 usiku na kwamba wao walianza kupokea majeruhi kuanzia majira ya saa tano kasoro na saa tano usiku.

Alisema kuwa walipokea wagonjwa nane ambao waliumia sana katika maeneo ya miguu ambapo alibainisha kuwa katika wagonjwa hao na ne kuna mmoja ambaye aliletwa akiwa na hali mbaya sana kitu ambacho kiliwalazimu kumfanyia upasuaji usiku huo huo.

“kati yawagonjwa hao nane mmoja alitwa akiwa mahututi sana kwani mguu wake ulikuwa umeadhiriwa sana na bomu hiloivyo ikatulazimu  kumkata mguu mmoja wa kushoto, kwakweli mgonjwa huyo ambaye tumemkata mguu anaitwa Deepak Gupta (25) mwanaume na sasa hivi anaendelea vyema kidogo, yupo katika chumba cha ICU ndani ya hospitali hii yetu ya Seliani”alisema Kisanga

Alisema kuwa  katika majeruhi au nane aliowapokea wanawake wako watatu huku wanaume wakiwa watano na kubainisha kuwa wote wameshafanyiwa upasuaji na wapo wodini kwa ajili ya uangalizi wa madaktari

Aidha aliwataja majeruhi hao kwa majina kuwa ni pamoja na  Vinod Suvesh(37), Ritwik Khandelval (13),Raj Rajin(30),Prateck Saver,manci Gupta(14) ,Manisha Gupta (36),Mahush Gupta(42) pamoja na Deepak Gupta (25)  wote wakiwa na asili ya kiasia

Kisanga alisema kuwa kwa mujibu wa wagonjwa hao walio  waliofika hapo hospitali walidai kuwa   bomu hilo lilirushwa kwa kupitia dirishani.

 

Hali ya usalama imezidi kuwa tete katika Jiji la Arusha kufuatia mfululizo wa matukio ya raia kujeruhiwa kwa kinachoaminiwa kuwa mabomu ya kurusha kwa mkono baada ya jana usiku kutokea mlipuka katika mgahawa wa kihindi ujulikanao kama Traditional Indian Cuisine uliopo maeneo ya Gymkhana Jijini hapa.

Taarifa zinaeleza kuwa watu wanane wamejeruhiwa huku wawili wakielezwa kuwa katika hali mbaya sana, huku mmoja aipoteza mguu wake kabisa. Majeruhi wamelazwa Selian Hospital.

picha ikionyesha askari wa jeshi la wananchi  kitengo cha mabom wakiwa katika eneo la tukio ambalo bumu lilirushwa  ndani ya mgahawa wa
ujulikanao kwa jina la Traditional Indian Cusine  ulipo pembeni ya hotel ya Gymkhana

www.woindeshizza.blogspot.com

mmoja wa mtu alielipuliwa na bomu katika mgahawa wa Traditional Indian Cusine aliyejukilana kwa jina la Deepak Gupta (25) akiwa amelazwa  katika hospitali ya Celiani ndani ya  chumba cha
mahututi (ICU) mara baada ya kukatwa mguu wake mmoja wa kushoto kutokana na mguu huo kuumizwa sana na bomu hilo

Mtoto   Manci  Gupta akiwa amelala anasikilizia maumivu ya miguu  aliyoumia mara baada ya kulipukiwa na bomu yeye na familia yao wakati wameenda kupata chakula cha usiku katika mgahawa huo

mama Munisha Gupta (42) pamoja na mme wake Mahush
Gupta (42) akiwa wameegemeana wote wamezurika katika mlipuko wa bomu
hilo wakati wameenda kupata chakula cha usiku

muonekano wa eneo la tukio

Sehemu ambayo inasemekana bomu  lilitua mara baada ya kutupwa

STORI NA PICHA: WINDE SHIZZA

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO