Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Diwani Bananga na Mbunge Mukya watoa msaada wa maturubai kwa kina mama wajasiriamali Sombetini

Mbunge wa Viti Maalum Arusha Mjini (CHADEMA) Mh Joyce Mukya  pamoja na Diwani wa Kata ya Sombetini Jijini hapa, Mh Ally Bananga (mwenye kombati ya khaki) hii leo wamagawa maturubai kwa kinamama wa soko la Mbauda lililoko Kata ya Sombetini ili yawasaidie kujikinga na jua wakati wa biashara zao sokoni hapo.

Kata hiyo ni miongoni mwa Kata ambazo Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kimefanya vizuri katika chaguzi zilizofanyika Disemba 14, 2014 kuchagua wenyeviti wa motaa na wajumbe wa Kamati  za mita. Chadema chini ya usimamizi wa Diwani Ally Bananga waliweza kujishindia jumla ya.mitaa 6 kati ya 8 iliyopo kwwnye Kata hiyo.

 
Diwani wa Kata ya Sombetini; Ally Bananga na Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA) Mh Joyce Mukya wakikabidhi msaada wa maturubai kwa kina mama wafanyabiashara
 
 
Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA) Mh Joyce Mukya akizungumza na waandishi wa habari
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO