Hakimu David Mwita wa Mahakama ya mwanzo ya Maji ya Chai ameahirisha hadi Disemba 24, shauri la kesi inayomkabili Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Mh. Joshua Nassari (CHADEMA), kwa tuhuma za kuharibu mali ya umma kwa kuichoma bendera ya CCM yenye dhamani ya shilingi laki mbili pamoja na kumteka mtu na kumtishia kwa bunduki tukio ambalo anatuhumiwa kufanya Disemba 15 mwaka huu
Mahakama hiyo imeweza kumuachia Mbunge huyo mara baada ya kutimiza mashariti ya dhamana ambapo shariti la kwanza ni kuwa na wadhamini wa tatu ambao wanamali zisizo hamishika zenye thamani ya shilingi milioni moja na nusu kila mmoja.
Katika kesi hiyo ambayo mlalamikaji wa kesi hiyo akiwa ni mtu binafsi, Hakimu wa kesi hiyo mara baada ya kusikiliza mashitaka hayo alichukuwa nafasi ya kuhairisha kesi hiyo hadi disemba24 ambapo kesi hiyo itatajwa tena kwa mara nyingine.
Akiongea mara baada ya kuairisha kesi hiyo Wakili wa mbunge huyo wa Arumeru Mashariki, James Ole Milya alisema kuwa amesikitishwa sana na tukio la Mahakama hiyo kumpa mashariti makubwa mteja wake kwani kesi yake ilikuwa haitaji mashariti makubwa hivyo .
Aidha alisema kuwa mbali na kupewa mashariti hayo angependa kesi hiyo ipelekwe katika Mahakama ya Wilaya ili yeye kama Wakili wa Mbunge huyo aweze kumtetea kwani katika Mahakama ya mwanzo hairuhuu kuweka wakili.
“unajua kwakweli mbali na hivyo pamoja kuwa sio Jamuhuri imemshitaki Mh Nasari bali ni mtu binafsi lakini nasikitika sana kwa mashariti ambayo wameweka ,kwani ata bila hao wadhamini watatu wakiwa na kitu kisichoamishikika chenye dhamani ya shilingi milioni moja na nusu,huyu ni Mbunge ambapo angeweza kujidhamini hata yeye mwenyewe kwani mtu huyu ni kioo cha jamii na hawezi kukimbia sehemu yoyote kwanini wasinge mpa mdhamana mapema mpaka apate wadhamini hawa na mashariti haya”alihoji Wakili Milya
Aidha Millya alisema kuwa anashangazwa sana na maamuzi haya kwani kuna mtu ambaye amemdhalilisha mwanamke ambaye alikuwepo Mahakamani hapo na akamvua mwanamke huyo nguo lakini yeye alishangazwa sana kwa mtuhumiwa wa kosa ilo la uzalilishaji yeye kupewa mashariti mapesi ya kuwa na mdhamini mmoja na kutoa laki tano laikini mbunge yeye amepewa mashariti ya kuwa na wadhamini watatu ambao wanamalizi zenye dhamani ya shilingi milioni moja na nusu huku akitilia shaka kuwa katika kesi hii wanahisi kuna chama cha siasa kinachangia kuongeza nguvu.
MAELEZO: WOINDE SHINZA
0 maoni:
Post a Comment