Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MASHINDANO YA MICHEZO YA WABUNGE WA AFRIKA MASHARIKI YAANZA JIJINI ARUSHA

unnamed

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akifurahia ushindi baada ya kushinda nafasi ya kwanza kupeperusha vema bendera ya Tanzania baada ya kuibuka mshindi  mbio za mita 100 akifuatiwa na Isaac Melley wa Kenya na Tom Aza wa Uganda aliyeshika nafasi ya tatu.

 SAM_0436

Maandamano ya mashindano ya michezo ya wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC),jijini Arusha ambayo yanatimua vumbi Uwanja Sheikh Amri Abeid  jijini Arusha kwanzia tarehe 6 hadi 12 mwezi huu

SAM_0464
Wabunge wa bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania wakifwatilia ufunguzi rasmi wa bonanza la mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kulia ni kiongozi wa timu ya bunge la Tanzania Idd Azan katikati ni Mh.mbunge Stevin Ngonyani a.k.a Maji marefu

SAM_0514

Wabunge wa Tanzania Halima Mdee na Ester Matiko waliendeleza ubabe wa bunge la Tanzania dhidi ya wenzao baada ya kushika nafasi ya kwanza na pili katika mbio za mita 1,500 na kuwaacha wenzao kutoka Uganda, Kiiza Winfred na Kangi Elizabeth wakishikilia nafasi za tatu na nne.

SAM_0498

Mbunge Ester Matiko wa Tanzania  akijiandaa kukimbia mbio za mita 400,ambapo aliwatimulia vumbi wabunge wenzake kutoka Kenya, Uganda na bunge la Afrika Mashariki (Eala).

SAM_0469

Kaimu Spika wa bunge la EALA Chris Opoka akizungumza katika ufunguzi wa mashindano hayo

SAM_0470

Mkuu wa wilaya Arumeru Mhe Nyirembe Munasa afungua mashindano ya michezo kwa wabunge ambapo aliwataka wachezaji kuacha kuamini imani za kishirikina na badala yake wamtegemee Mungu kwani michezo ni kazi kama ajira nyingine

SAM_0440SAM_0452

SAM_0495

Mkurugenzi wa KeyMedia Agency Limited Bi Anna Lazaro akiwa na wabunge wa Tanzania leo jijini Arusha katika mashindano ya michezo mbalimbali yaliyoandaliwa na EALA(East African Legislative Assembly)

SAM_0508

Katikati Mkurugenzi wa KeyMedia Agency Limited Bi Barbra Lazaro akiwa na wabunge wa Tanzania leo jijini Arusha katika mashindano ya michezo mbalimbali yaliyoandaliwa na EALA(East African Legislative Assembly)

SAM_0559

Aliyevalia t-shart ya njano ni designer mkuu wa kampuni ya KeyMedia Agency Limited Bahati Masawe akiwa na waheshimiwa Wabunge

SAM_0553

Mbunge wa EALA kutoka nchini Tanzania Mh.Twaha Taslama akiwa anavuta kamba wakati wa mashindano ya hayo

SAM_0489

Mbunge wa Kenya akiwa amebebwa juju baada ya kushinda katika mbio za mita 100

SAM_0494

Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mkoa wa Mara, Ester Bulaya akiwa anashangilia kwa furaha katika mashindano hayo

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO