Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA) Mh Ester Matiko amesherehekea Siku Kuu ya Krismasi pamoja na watoto waishio katika mazingira magumu Tarime Mkoani Mara na kupata chakula pamoja kama sehemu ya Shukurani yake kwa Mungu kwa kumnusuru na ajali mbaya yeye na watoto wake majuma kadhaa yaliyopita.
Mh Matiko alijitolea ng’ombe, mchele kilo 100, soda maji na juice ambavyo ndivyo vilitumika kwa shughuli hiyo na watoto wakala na kunywa na kufurahia sikukuu
Sambamba na tukio hilo la chakula cha pamoja, kulikuwa na michezo mbalimbali kwa watoto hao kama kukimbia mbio fupi, kukimbiza kuku, kucheza muziki n.k na kuhitimishwa jioni na mechi kabambe ya mpira wa miguu baina ya MABOGI FC na MWEMA FC katika raundi ya nane ya michuano ya ESTER MATIKO FOOTBALL RISING CUP, vyote vikifanyikia katika uwanja wa Tarime.
Kwa michezo ya watoto wanaoishi katika mazigira magumu, washindi walipatiwa zawadi mbali mbali zikiwemo fedha taslimu kutoka kwa mbunge huyo.
Mh Ester Matiko, Mbunge Viti Maalumu (CHADEMA) akipatiwa chakula katika siku ya Krismasi, chakula alichoandaa kula pamoja kusherehekea sikukuu na watoto waishio katika mazingira magumu ndani ya mji wa Tarime na maeneo jirani
Mechi kabambe baina ya Mabogi FC na Mwema FC ikiendelea katika raundi ya nane ya michuano ya ESTER MATIKO FOOTBALL RISING CUP. Mechi hiyo iliyanfyika jioni baada ya shughuli ya sikukuu na watoto uwanja wa Tarime ambapo Mwema FC waliwafunga Mabogi FC kwa jumla ya magoli 3 kwa 1.
PICHA ZOTE NA: ESTER MATIKO
0 maoni:
Post a Comment