Diwani pekee wa kuchaguliwa wa chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Michael Kivuyo wa Kata ya Sokoni 1 Mkoani Arusha amevuliwa uanachama kwa kile kinachodaiwa kushindwa kusimamisha wagombea wa chama chake kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Jumapili kesho Disemba 14, 2014.
Uamuzi huo umechukuliwa na Kamati ya Utendaji ya TLP Wilaya ya Arusha Mjini baada ya kikao cha Sekretaieti ya chama hicho kuka Novemba 20 na kuamua hivyo.
Mwenyekiti wa TLP WIlaya ya Arusha Bw Deogratius Makishe akiongea na wanahabari alitangaza tuhuma tano kwa Kivuyo kuwa ni
1. Kushindwa kusimamisha wagombea wa Serikali za Mitaa
2. Kuhamasisha viongozi wa Serikali za Mitaa kwa tiketi ya TLP na kuwashawishi kugombea kupitia NCCR-Mageuzi
3. Kufanya kazi ya kuijenga NCCR –Mageuzi badala ya TLP 4 ambacho yeye ni Diwani wake
4. Kutotoa ushirikiano kwa viongozi wa TLP Wilaya na
5. Madai kwamba kwasasa Kivuyo ni mwanachama wa NCCR wakati ni Diwani kupitia TLP
0 maoni:
Post a Comment