Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

KUMBUKUMBU: WABUNGE WA TANZANIA WALIOFARIKI KWA AJALI

Wabunge

Wabunge wa Tanzania waliokufa kwa ajali, iwe ndege, gari au usafiri wowote ule!

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime (Chadema), marehemu Chacha Zakayo Wangwe enzi za uhai wake.

Hussein Ramadhan Shekilango; alikuwa Mbunge wa Jimbo la Korogwe (CCM) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (utawala). Alifariki dunia Mei 11, 1980 kwa ajali ya ndege iliyotokea kwenye milima ya Arusha. Kumuenzi, serikali iliipa jina Barabara ya Shekilango iliyopo Sinza, Dar.

Juma Jamaldin Akukweti; alikuwa Mbunge wa Jimbo la Tunduru (CCM) na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge). Alifariki Januari 4, 2007 Hospitali ya Johannesburg, siku chache baada ya ajali ya ndege iliyoanguka ikitaka kupaa Desemba 16, 2006 jijini Mbeya alikokuwa kwa shughuli za kikazi.

Aliyekuwa Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Jimbo la Uzini, Zanzibar, Mussa Khamis Silima enzi za uhai wake.

Chacha Zakayo Wangwe; alikuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime (Chadema). Alifariki dunia papo hapo kwa ajali mbaya ya gari dogo aina ya Toyota Corolla iliyotokea maeneo ya Kongwa, Dodoma, saa 2: 55 usiku wa Julai 27, 2008 akiwa njiani kuelekea msibani Dar.

Salome Joseph Mbatia; alikuwa Mbunge wa Viti Maalum-CCM na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto. Alifariki papo hapo Oktoba 23, 2010 katika ajali mbaya ya gari lake aina ya Nissan Patrol kugongana uso kwa uso na Fusso maeneo ya Kibena, akiwa njiani kwenda Njombe.

Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum-CCM na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Salome Joseph Mbatia enzi za uhai wake.

Regia Estelatus Mtema; alikuwa Mbuge wa Viti Maalum (Chadema). Alifariki dunia kwa ajali ya gari aina ya Toyota Land Cruiser iliyotokea maeneo ya Ruvu Darajani, Mkoa wa Pwani Januari 14, 2012 akiwa njiani kutoka Dar kwenda Ifakara kukagua kiwanja alichopewa na wazazi wake.

Mussa Khamis Silima; alikuwa Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Jimbo la Uzini, Zanzibar. Alifariki katika ajali ya gari Agosti 23, 2011 maeneo ya Nzuguni, Dodoma pamoja na mkewe, Mwanaheri Fahari. Marehemu alikuwa akielekea bungeni Dodoma kutokea Dar.

Aliyekuwa Mbuge wa Viti Maalum (Chadema), Regia Estelatus Mtema enzi za uhai wake.

Edward Moringe Sokoine; alikuwa Mbunge wa Jimbo la
Monduli (CCM) na Waziri Mkuu wa Tanzania. Alifariki kwa ajali Aprili 12, 1984 eneo la Dumila, Morogoro. Ili kumuenzi, serikali imetoa jina la Barabara ya Sokoine, ipo Posta jijini Dar na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, Morogoro.

 

CHANZO: MOSHONO MEDIA

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO