Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Kutoka Arumeru: Ofisa Mtendaji Kata aahirisha kesi ya Joshua Nassari

Kesi ya kuchoma moto bendera ya CCM inayomkabili Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari (pichani) jana iliahirishwa na Ofisa Mtendaji wa Kata ya Maji ya Chai, Ndikilo Mbise kutokana na Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ya Maji ya Chai, David Mwita kuwa safarini.

Akiahirisha kesi hiyo, Mbise alisema itatajwa tena Januari 20 mwakani.Mbise alisema Hakimu Mwita amepata msiba, hivyo amekwenda nyumbani kwao mkoani Mara huku, hakimu mwingine wa mahakama hiyo akiwa likizo.

Mbise alisema ameahirisha kesi na kuipangia tarehe nyingine kwa kuwa ni mlinzi wa amani wa eneo hio.

Katika kesi hiyo, Nassari ambaye hakuhudhuria mahakamani hapo kutokana na kuwa safarini, anatuhumiwa kuchoma bendera ya CCM Desemba 15, saa 11 jioni katika eneo la Maji ya Chai. Bendera hiyo yenye thamani ya Sh250,000 ilikuwa mali ya Raphael Moses.

Ilielezwa mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa ataendelea kuwa nje kwa dhamana ya wadhamini watatu ya Sh1.5 milioni kila mmoja.

 

Source: Mwananchi-25/12/2014

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO