Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

KUTOKA ARUSHA: DKT. BILAL AMTUNUKU SHAHADA YA UZAMIVU RAIS KIKWETE

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimtunuku shahada ya heshima ya Uzamivu (PhD) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Profesa Jakaya Mrisho Kikwete, kwa kutambua mchango wake katika Jamii, kitaifa na kimataifa pamoja na kufanikisha kuanzishwa kwa Taasisi hiyo. Dkt Jakaya alitunukiwa Shahada hiyo wakati wa Mahafali ya pili ya Taasisi hiyo yaliyofanyika leo Jijini Arusha.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambae pia ni Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimtunuku shahada ya Sayansi Uhandisi na Hesabu PhD, James Philip, wakati wa Mahafali ya 2 ya Taasisi hiyo iliyofanyika leo jijini Arusha.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia kwenye Mahafali ya 2 ya Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela iliyofanyika leo jijini Arusha.

Baadhi ya wahitimu...

Baadhi ya wahitimu...

Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake ambaye ni Mkuu wa Taasisi hiyo, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu.

Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake ambaye ni Mkuu wa Taasisi hiyo, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika maandamano na viongozi wa Taasisi hiyo pamoja na wahitimu, wakati wa Mahafali ya 2 ya Taasisi hiyo yaliyofanyika leo jijini Arusha. Picha na OMR

Washirikishe Google Plus

About Ujenzi Connekt

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO