Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

WAFUGAJI WAATHIRIWA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI

ngombe
Picha ya makataba
****

Na Ferdinand Shayo,Arusha.

WAFUGAJI kutoka Wilaya za Ngorongoro ,Longido na Monduli wameeleza kuanza kukumbwa na athari za matokeo ya mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi.

Wakizungumza katika kongamano la jamii za kifugaji zinazoishi katika nyanda kame lililoandaliwa na shirika la Haki kazi Catalyst na taasisi ya kimataifa ya mazingira na maendeleo (IIED) viongozi wa jamii hiyo walisema kuwa tayari wameanza kukosa mvua za kutosha katika maeneo yao

“ Joto limekuwa kali sana, mvua hazitabiriki ,tunashindwa kujua misimu tuliyozea,wakati mwingine mvua kubwa inanyesha kiasi cha kuleta hofu na mafuriko makubwa tofauti na siku za nyuma ,hali hii ni ishara kuwa hali ya siku zijazo ni tete”alisema Martalo.

Diwani wa viti maalum kutoka Wilaya ya Ngorongoro Tina Timan alisema kuwa kwa sasa wanawake wa jamii hizo wanasafiri umbali kutafuta maji kufuatia vyanzo vya maji kukauka kufuatia hali ya ukame.

“Nimefurahi kwa mpango huu na hasa kutokana na kushirikisha wanawake wa jamii za kifugaji ambao ndio wahanga wakubwa wa tatizo hili ,sisi ndio tunasafiri mbali kufuata maji ,kutafuta kuni ” .anasema Tin

.

Tina aliongeza kuwa migogoro ya ardhi na sera mbalimbali zinawaweka wafugaji katika hatari zaidi ,maeneo yao yanachukuliwa na kugeuzwa hifadhi na mengine kupewa wawekezaji tunaomba katika mikakati hii hili nalo litazamwe.

Esupat Ngulupa kutoka Longido alisema kuwa miaka michache iliyopita wafugaji walipoteza idadi kubwa ya mifugo baada Wilaya hiyo kukumbwa na ukame uliodumu kwa muda mrefu.

“Tunashukuru mashirika haya kujitokeza kutuelimisha namna ya kupambana athari zitokanazo na mbadiloko ya hali ya hewa na tabia nchi”alisema Esupat.

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi huo kutoka taasisi ya kimataifa ya mazingira na maendeleo (IIED)Alais Morindat alisema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia jamii hiyo kuweka mikakati na mipango ya kukabili athari za mabadiliko ya tabia nchi.

“Kila Wilaya ina mratibu ambaye pamoja na wawakilishi wa jamii katika Wilaya husika wataweka mipango ya kukabiliana na matokeo ya tatizo hili’alisema Morindat.,

Alisema kuwa jamii pamoja na viongozi wa kisiasa ilishiriki kikamilifu katika kongamano hilo na kutoa mawazo na uzoefu, kutafakari kwa pamoja sera na dira ya maendeleo ya taifa katika kuondoa umaskini na jitihada za taifa katika kukabili mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi.

Aidha Morindat aliongeza kuwa washiriki pia walijadili kwa undani masuala ya msingi juu ya dhana na Sayansi ya mabdiliko ya hali ya hewa na tabia Nchi pamoja na Mifumo ya wafugaji iliyopo na inayopotea katika kuhimili mabadiliko mbalimbali yanayotokea.

Sera na sheria za nchi na jinsi inavyowezesha ama kutowezesha mifumo hiyo ya kijamii kufanya kazi na mabadiliko makubwa ya kiuchumi duniani faida na athari zake kwa mifumo ya Kijamii.

Washirikishe Google Plus

About Ujenzi Connekt

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO