Mawasiliano ya internet nchini Korea Kaskazini yamerejea leo Jumanne baada ya kupotea kwa zaidi ya saa tisa.
“Ni kama vile Korea Kaskazini ilifutwa kwenye ramani ya dunia ya Internet,” Rais wa kampuni ya masuala ya usalama iitwayo, CloudFlare, Matthew Prince aliiambia CNN.
Tatizo hilo limekuja wakati ambapo Korea Kaskazini na Marekani zipo kwenye vita vya maneno kufuatia kushambuliwa kimtandao kwa kampuni Sony Pictures. Marekani inaishutumu Korea Kaskazini kuwa imehusika japo yenyewe imekanusha.
Korea imechukizwa na filamu ya ‘The Interview’ inayosimulia kisasa cha kutunga cha mpango wa kuuawa kwa kiongozi wake, Kim Jong Un.
Kampuni ya Sony iliamua kusitisha kuizindua filamu hiyo kufuatia vitisho vya kigaidi kwenye majumba ya sinema.
0 maoni:
Post a Comment