Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MAKAMU WA RAIS WA JICA AMTEMBELEA WAZIRI WA UJENZI OFISI KWAKE JIJINI DAR ES SALAAM

magufuliMakamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Japan JICA, Kato Hiroshi akimueleza jambo Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu masuala mbalimbali yahusuyo Sekta ya Ujenzi wa barabara nchini wakati alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akifafanua jambo kwa Makamu wa Rais wa JICA Kato Hiroshi.

Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Gerson Lwenge ( wapili kulia), akimuuliza swali Makamu wa Rais wa JICA Kato Hiroshi (wa kwanza kushoto) kuhusu miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Serikali ya Japan kupitia Shirika hilo la Maendeleo.

Baadhi ya wajumbe kutoka JICA wakiangalia baadhi ya picha za matukio mbalimbali katika Wizara ya Ujenzi kabla ya mkutano wao na Waziri wa Ujenzi.

Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa Rais wa JICA, Kato Hiroshi mara baada ya kumaliza mkutano wao uliofanyika Wizara ya Ujenzi.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO