Wachezaji wa Tanzania na Kenya wakiwa katika mashindano ya wabunge wa jumuiya ya Afrika mashariki leo, katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Karume jijini Arusha, mechi hiyo ilivuta hisia za wakazi wa jiji hilo waliomiminika kuja kushuhudia wabunge hao wakimenyana uwanjani, baada ya dakika ya tano bunge la kenya walijipatia bao la kwanza, bao lililofungwa na Mh.Steven Nyatta na hatimaye Tanzania kusawazisha dakika ya 24 kwa njia ya penalt baada ya Mh.Mbunge Joshua Nassari kudondoshwa eneo la hatari kwa kugongwa na mlinda mlango wa kenya Kega Kanin.
Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Mh Iddi Azan mlinda malango ambaye pia ni kiongozi wa timu ya bunge la Tanzania akinyaka magoli akionyesha umahiri wake wa kudaka mpira hali iliyosababisha mashabiki wa jiji la Arusha kumshangilia
Mlinda mlango wa Timu ya kenya Kega Kanin akijaribu kuzuia goli lililopatikana kwa njia ya penalt katika dakika ya 24
Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima akichechemea uwanjani baada ya kuanguka na kupewa huduma ya kwanza
Wachezaji wa timu ya Tanzania wakijadiliana uwanjani kabla ya mechi kuanza
Wachezaji wa timu ya Kenya wakijadiliana uwanjani kabla ya mechi kuanza
Kushoto ni mchezaji wa timu ya kenya Mh.Peter Kaluma katikati ni Mh Dan Wanyama wa kenya mrefu kuliko wote uwanjani alipewa kadi nyekundu baada ya kuonekana akijibizana na mwamuzi aliyekuwa akichezesha mpambano huo kulia ni Mh Joshua Nassari wa Tanzania
Kushoto Mh Iddi Azan ambaye ni mlinda malango wa timu ya Tanzania akiwa katika mapumziko, aliyeshikilia mpira ni mwamuzi wa mpambano huo Erick OnokoMh Joshua Nassari wa Tanzania akipewa huduma ya kwanza
Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima akipatiwa huduma ya kwanza
Mh.Mbunge wa Tanzania akiwa amelala chali akionekana kuwa na maumivu makali baada ya kuumia katika mechi hiyo wabunge wenzake wakijaribu kumsaidiaMashabiki wa Kenya wakiwa wanashangilia huku wakiwa wanaonyesha bwebweeee zao
Umati wa watu waliokuja kushuhudia mpambano wa Tanzania na Kenya
Mashabiki wa Tanzania wakiwa wanashangilia kwa kuzunguka uwanja
Watoa huduma ya kwanza kutoka msalaba mwekundu wakiwa wanafatilia mechi ya wabunge wa Afrika mashariki
WAKATI HUO HUO.. PAMELLA MOLEL ANARIPOTI KWAMBA
TIMU YA EALA IMEICHAPA BURUNDI 4-2
(Wachezaji wa Timu ya EALA waliovalia jezi rangi ya blue wakipambana na wenzao timu ya Burundi)
Timu ya wabunge wa EALA wameicharaza mabao manne kwa mbili timu ya Burundi jana katika Uwanja Sheikh Amri Abeid jijini Arusha ikiwa ni muendelezo wa mashindano ya wabunge Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)
Mchezaji mahiri wa timu ya Eala John King aliipatia mabao 3 timu yake dakika ya 9 na 21 kipindi cha kwanza hali iliyosabaisha mashabiki waliomiminika katika uwanja huo kumshangila
Kipindi cha pili hali ilibadilika baada ya timu ya Burundi kujipatia mabao mawili dakika ya nne na dakika ya 18, mpigaji wa magoli hayo ni Simon Gahinja
Baada ya mchuano mkali wa timu zote mbili ,Eala waliongeza bao la 4 lililofungwa na mchezaji Wilyclif Keto dakika ya 25 baada ya kupata penalt dakika 33 ambapo mpigaji penalt alikosa baada ya mlinda mlango wa Burundi Ibrahim Uwizey kudaka
Mbunge wa EALA kutoka nchini Tanzania Mh.Twaha Taslama jezi namba 12 akiwa uwanjani
Mh Mbunge wa Eala Bernad Mrunya akiwa anajiandaa kukabilia na timu ya Burundi katika Uwanja Sheikh Amri Abeid jijini Arusha ikiwa ni muendelezo wa mashindano ya wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)
0 maoni:
Post a Comment