Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MHE.RAIS KIKWETE AONGOZA SHEREHE ZA KUTUNIKIWA KAMISHENI MONDULI

Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Waziri Mkuu wa Mstaafu Mhe Edward Lowassa walipohudhuria sherehe za kutunukiwa kamisheni maofisa wapya wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa cheo cha Luteni Usu, iliyofanyika katika chuo cha jeshi hilo Monduli, mkoani Arusha leo.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa akiongea na maofisa waandamizi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania akiwemo na Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange (kushoto) kwenye sherehe za kutunukiwa kamisheni maofisa wapya wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa cheo cha Luteni Usu, iliyofanyika katika chuo cha jeshi hilo Monduli, mkoani Arusha leo

Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akimkaribisha Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa alipowasili kwenye sherehe za kutunukiwa kamisheni maofisa wapya wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa cheo cha Luteni Usu, iliyofanyika katika chuo cha jeshi hilo Monduli

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa (kulia) akizungumza na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi walipohudhuria sherehe za kutunukiwa kamisheni maofisa wapya wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa cheo cha Luteni Usu, iliyofanyika katika chuo cha jeshi hilo Monduli

Maofisa wapya wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa cheo cha Luteni Usu wakila kiapo cha utii mbele ya Rais Jakaya Kikwete baada ya kutunukiwa kamisheni katika chuo cha jeshi hilo Monduli, mkoani Arusha

Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akiongea na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa kwenye sherehe hizo

Burudani katika sherehe hizo

Maofisa wapya wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa cheo cha Luteni Usu wakitembea kwa ukakamavu walipokuwa wakitoa heshima kwa Rais Jakaya Kikwete katika sherehe za kutunukiwa kamisheni maofisa hao, Monduli, mkoani Arusha

Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akiongea na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Daudi Felix Ntibenda

Wimbo wa Taifa ulipopigwa

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO