Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

WANANCHI MTAA WA MIGOMBANI WAMWAPISHA MWENYEKITI SERIKALI YA MTAA SEGEREA KWA KUTUMIA WAKILI BINAFSI

chadema_kuapishwa

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Migombani-Segera, Japhet Albert Kembo akiapishwa jana jijini Dar es Salam.

*****

Baada ya kusubiri kwa muda wa wiki mbili ili wajumbe serikali ya mtaa wa Migombani-Segerea waapishwe na mamlaka husika bila mafanikio, wananchi wameamua kuwaapisha viongozi hao kwa kutumia wakili binafsi.

Tukio hilo limetokea jana asubuhi katika ofisi za Serikali za Mitaa zilizopo Segerea Mwisho ambalo lilijumuisha kuapishwa kwa Mwenyekiti wa Mtaa, Japhet Albert Kembo pamoja na wajumbe watatu ambao ni Rose Benard Mhagama, Nyangeto Flora Justin na Ramadhan Rashid Seif.

Akizungumza baada ya kuapishwa, mwenyekiti mpya wa mtaa huo amesema kuwa wananchi wamechoshwa na danadana wanazopigwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala za kutowaapisha viongozi waliowachagua ndiyo maana wamefikia hatua hiyo ili kuwakumbusha kutekeleza majukumu yao kwa wakati.

“Wananchi wanahitaji huduma kutoka kwa watu wanaowaamini lakini wanakosa imani pale uongozi wa manispaa unaposhindwa kutekeleza majukumu yake kama inavyotakiwa kwa mujibu wa sheria. Wamemtafuta wakili ambaye amekuja kulisimamia suala hili kisheria na ndiyo maana zoezi limefanywa hadharani,” alisema Kembo.

Wananchi waliozungumza walisema kuwa hawaelewi kinachoendelea kwakuwa uchaguzi ulifanyika kama kawaida pasipo dosari yoyote na matokeo yakatangwazwa huku nafasi zote zikichukuliwa na wagombea kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

“Uchaguzi wetu haukuwa na matatizo na ni miongoni mwa mitaa iliyotangaza matokeo muda mfupi baada ya uchaguzi kufanyika lakini jambo la kushangaza ni kwamba viongozi wote waliochaguliwa hawajaapishwa kama ilivyofanyika kwa wengine katika manispaa hii wakati hakuna pingamizi lolote mahakamani linalozuia uhalali wa waliochaguliwa,” alisema John Kandeo, mmoja wa wananchi walioshuhudia kuapishwa kwa viongozi hao.

Akifafanua kuhusu matokeo ya uchaguzi uliofanyika Desemba 14, mwaka jana, Kembo alisema kuwa walikuwa wagombea watatu katika nafasi ya uenyekiti ambao ni yeye mwenyewe aliyepata jumla ya kura 547, Uyeka Idd wa CCM aliyepata kura 273 na Erick Mchata wa NCCR-Mageuzi aliyepata kura 205.

Zoezililivyokuwa

Muda wa saa 05:00 asubuhi, wakili wa kujitegemea kutoka kampuni ya mawakili ya Ame and Company, Idd Msawanga aliwasili katika ofisi za mtaa huo na kupokelewa kwa kelele nyingi za wafuasi wa Chadema waliokuwa wakipaza sauti zao kwa sauti kubwa za ‘Peoples…Power.’

Wakili Msawanga alianza kwa kumuapisha mwenyekiti, peke yake, na baadaye wajumbe hao watatu kwa pamoja na kuelezwa kuwa wajumbe wawili hawakuwepo kutokana na matatizo ya kifamilia.

“Sheria ya uchaguzi inaruhusu kufanya hivi na hata hao wajumbe wawili ambao hawapo kwa leo watakaporudi nitawaapisha…ni suala la kutaarifiana tu,” alisema Msawanga.

 

Chanzo: Mitandao ya kijamii

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO