Kile kinachotafsiriwa kuwa mgomo wa waendesha magari madogo ya kubeba abiria kwa Jiji la Arusha maarufu kama “vifodi” umeendelea tena hii leo ikiwa ni siku ya pili mfululizo kwa baadhi ya njia. Kwa mfano kwa njia ya kutoka maeneo ya Moshono kuelekea mjini hakuna gari yeyete ya abiria kabisa, halikadhalika njia itokayo Njiro kwenye mjini pia.
Wasafiri wa njia hizo wamejikuta wakilazimika kusafiri katika mazingira ya hatari kwa kujazana kwenye magari ya wazi na pikipiki za mizigo vyombo ambavyo si maalumu kwa ubebeaji wa abiria.
Uchunguzi wa Blog hii umegundua kuwa wanaosababisha zaidi hali hii ni wapiga debe ambao wanaona kwa mfumo mpya wa hizi njia za usafiri kama mpango wa Jiji kukabiliana na msongamano barabarani hawataweza kupata ujira wa kuitia abiria kwenye magari, na hivyo baadhi yao kuwafanyia vurugu madereva wanaotaka kufanya kazi. Lakini pia kuna baadhi ya madereva ambao ni kama hawauelewa utaratibu huo mpya na kujikuta wakigoma kuendesha magari yao.
Picha zifuatazo zinasimualia baadhi ya matukio barabarani.
Home
ARUSHA NEWS
HABARI
“Mgomo” wa Daladala Arusha Waingia Siku ya Pili kwa Baadhi ya Njia, Wasafiri Walazimika Kupanda Guta, Pick Up na Canter Kwenda Kazini
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 maoni:
Post a Comment