Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Freeman Mbowe atoa magari ya wagonjwa Hai

Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA, Mbunge wa Jimbo la HAI,,na Kiongozi wa kambi RAsmi bungeni MH FREEMAN MBOWE ameendeleza juhudi zake katika kuokoa maisha wa watu wa jimbo lake ambapo wiki hii ametoa ambulances kwa ajili ya watu wa jimbo lake la Hai.
Kutolewa kwa ambulance hiyo itakuwa ni ukombozi mkubwa kwa wakazi wa HAI jimbo ambalo limetawaliwa na mito na mabonde mbalimbali ambapo litatumika kuwawaisha wagonjwa hospitali za teule ya Machame na ile ya Wilaya.

Kufuatia kutolewa kwa ambulance hiyo mkazi mmoja wa kata ya Machame Mashariki(LYAMUNGO KATI) amesema itakuwa ni msaada mkubwa sana kwao maana itarahisisha kupeleka wagonjwa kutoka Kituo cha afya Lyamungo Hadi hospitali teule ya Machame.
Baadhi ya wakazi wa Masama(Masama Bweera) wameonekana kufurahia na wengine kudiriki kusema kama FREEMAN MBOWE atagombea tena watampa ushiindi wa kishindo kutokana na mheshimiwa Mbowe kutoa Ahadi zake bila kupendelea upande wowote.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO