Wakazi wa Jijini Arusha na maeneo ya Jirani wamekubwa na kadhia ya kukosa magari ya kusafirisha kuingia na kutoka mjini asubuhi ya leo baada ya kutokea mgomo wa waendesha magari ya abiria Jijini maarufu kama Vifodi wakisusia njia mpya za usafiri Jijini hapa.
Blog hii iliweza kushuhudia wananchi wengi hasa kutoka maeneo ya Njiro na Moshono wakilazimika kutembea kwa miguu umbali mrefu na waliojimudu walichukua ‘bodaboda’ kuwawahisha makazini na wengine kwenda mjini kwa shughuli nyingine za kila siku.
Maeneo ya stand mjini kulikuwa na vurugu za baadhi ya wapiga debe walikazimisha madereva kukaidi kufuata njia hizo mpya zilizopitishwa na Sumatra zikitarajiwa kuanza kutumika rasmi hii leo. Moja ya njia hizo ni kuanzisha njia ya kutoka Njiro mpaka Kisongo na kKwa Morombo ambapo baadhi zinapitia Philips hadi Kisongo na nyingine zinachepukia ilipo Hoteli ya East Africk na kutokea Unga Ltd.
Muda wote huo askari wa usalama barabarani na wale mgambo wa Jiji walikuwa wamejigawa maeneo tofauti yenye maunganikio ya njia kulingana na mabadiliko hayo.
0 maoni:
Post a Comment