Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Jimbo la Arusha Mjini kimeanza hii leo kuendesha semina za kuwapa muongozo wa kiutendaji kama viongozi wapya wa chama hicho, Wenyeviti na Wajumbe wao walioshinda kuongoza Serikali za Mitaa kupitia chama hicho.
Mafunzo hayo yameanza rasmi hii leo katika hotel ya kitalii ya New Arusha ya Jijini hapa na yanatarajiwa kuendelea tena kesho.
Chadema ilishinda jumla ya mitaa 76 kati ya 155 iliyoorodheshwa kufanya chaguzi na kati ya hiyo mitaa mitano haikuwa na uchaguzi baada ya wagombe wa Chadema kuenguliwa kwa sababu mbalimbali na kuachia wagombea wa CCM kupita bila kupingwa.
Aidha Chadema ina mitaa 5 ambayo wajumbe wote wa Serikali wanatokana nayo lakini wenyeviti ni wa CCM ambayo ilishinda mitaa 73 na hiyo mitano bila kupingwa.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Chadema, Chadema wanaumiliki wa mabaraza ya maamuzi katika Kata 11
Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema (CHADEMA) akizungumza katika semina hiyo
Baadhi ya wenyeii na wajumbe wa Serikali za Mitaa watokanao na CHADEMA katika Jiji la Arusha wakisikiliza semina kwa makini
Mtoa mada Innocent Kisanyage akionekana kufafanua jambo wakati wa semina hiyo
0 maoni:
Post a Comment