Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

SAUDIA ARABIA NA TANZANIA WAANZA KUSHIRIKIANA KATIKA UHIFADHI WA WANYAMAPORI

Ujumbe wa Serikali ya Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb) katika mazungumzo na Mwana wa Mfalme wa Saudia Prince Bandar bin Saud bin Mohammad Al-Saud ambaye pia ni Rais wa Mamlaka ya Wanyamapori ya Saudi Arabia. Wengine katika picha kutoka kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Adelhem Meru; Balozi wa Tanzania Saudi Arabia Prof. Abdillah Omari; Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe. James Lembeli; Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii Mhe. Peter Msigwa; Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi;Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Herman Keraryo na Afisa wa Ubalozi Ndg. Sufian.

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb) akisisitiza jambo katika mazungumzo na Mwana wa Mfalme wa Saudia Prince Bandar bin Saud bin Mohammad Al-Saud ambaye pia ni Rais wa Mamlaka ya Wanyamapori ya Saudi Arabia.

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Adelhem Meru (kati) akiongea katika mazungumzo baina ya ujumbe wa Tanzania na Saudi Arabia. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe. James Lembeli na kushoto ni Balozi wa Tanzania Saudi Arabia Prof. Abdillah Omari.

Mwana wa Mfalme wa Saudia Prince Bandar bin Saud bin Mohammad Al-Saud ambaye pia ni Rais wa Mamlaka ya Wanyamapori ya Saudi Arabia akiongea katika mazungumzo hayo.

Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi akichangia jambo katika mazungumzo hayo. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Herman Keraryo; Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii Mhe. Peter Msigwa; Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe. James Lembeli na Balozi wa Tanzania Saudi Arabia Prof. Abdillah Omari.

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (wa tatu kushoto) ukiwa katika picha ya pamoja na Mwana wa Mfalme wa Saudia Prince Bandar (wa nne kushoto) jijini Riyadh, Saudi Arabia. Wengine kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania Saudi Arabia Prof. Abdillah Omari; Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Adelhem Meru; Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii Mhe. Peter Msigwa; Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe. James Lembeli; Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Herman Keraryo.

Ujumbe wa Mwana wa Mfalme wa Saudi Arabia ukifuatilia mazungumzo hayo.

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (kulia) akiwa na mazungumzo na (kutoka kulia) Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Adelhem Meru; Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe. James Lembeli na Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii Mhe. Peter Msigwa muda mfupi kabla ya kuanza kwa mazungumzo baina ya Tanzania na Saudi Arabia jijini Riyadh, Saudi Arabia.

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO