Taarifa kutoka Manispaa ya Moshi zilizoifikia Blog hii muda huu zinaeleza kuwa Kikao cha Bajeti ya Hamlashauri hiyo kimeshindwa kuamua haima ya bajeti husika mapema leo asubuhi baada ya Madiwani walio wengi wa Chadema wakiongozwa na Meya Jaffari kugomea kupitisha bajeti hiyo kwa madai kwamba Mkurugenzi wa Hamlashauri hiyo anatakiwa arudishe kwanza kiwanja cha umma (open space) anayodaiwa kushiriki kummilikisha kwa mtu binafsi.
Mkurugenzi huyo Bw Shabani Ntarambe anadaiwa kumuagiza afisa mipango miji wa Manispaa hiyo kuandaa hati ya umiliki wa kiwanja kilichoelezwa kuwa cha umma kwa mtu binafsi (Mawenzi SPort Club). Kiwanja hicho ni eneo lililopo jirani na Kituo Kikuu cha Polisi ambako ndipo zilipo Osifi za Kata na Tarafa ya Mawenzi na viongozi wote wa Kata na Tarafa wanaitumia ofisi hiyo.
Kwa mujibu wa maelezo ya Diwani Hawa Ali wa Manispaa hiyo, inadaiwa kuwa walifanya uchunguzi baada ya kupata tetesi za mpango wa kugawa eneo hilo kwa mtu binafsi na wakaweka kizuizi lakini baadae wakagundua kuwa Mkurugenzi amamuagiza mwanasheria kuondoa zuio hilo na hatimaye mtu huyo aliyemilikishwa “Mawenzi Sport Club” kupatiwa hati ya umiliki jana. na kwamba ni kiwanja ambacho kilishatangazwa kama eneo la uwekezaji.
Blog hii inaendelea kufuatilia sakata hilo na kukujuza zaidi mauziano hayo yalikuwaje na mmiliki halali hasa ni nani!
Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa a Moshi Mjini wakitoka nje ya Ukumbi wa Mkutano baada ya kugoma kuitisha bajeti hiyo hii leo asubuhi
Meya wa Manispaa ya Moshi, Diwani Jaffari
Madiwani na wanahabari wakiwa nje ya lango la Ofisi ya Manispaa ya Moshi
0 maoni:
Post a Comment