Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Khalid, Athanas na Juma Waliotaka Kwenda Ikulu Tokea Geita Kwa Miguu Waishia Kukamatwa na Polisi Dar es Salaam

SRRRRRR

VIJANA watatu pichani; Khalid Selemani, Athanas Michael na Juma Maganga wanaoaminika kuwa ni wafuasi wa Chama Kikuu cha Upinzani CHADEMA, wamekamatwa na Polisi eneo la Magomeni Mapipa Jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Januari 2, 2014, baada ya dhamira yao ya kutembea kutoka Mkoa wa Geita wakielekea Ikulu ya Dar es Salaam kumuona Rais Jakaya Kikwete kufikisha ujumbe wao kuishia hapo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa Wilaya Kinondoni Jijini Dar es Salaam, Jordan Rugimbana, vijana hao watatu, Juma Maganga, Khalifa Selemani na Athanas Michael, walielekezwa na maafisa usalama kumuona yeye DC baada ya kuwasili kwenye eneo lake la utawala wakitokea Geita, ili awape baraka za kwenda Ikulu. Lakini walipofika ofisini hapo, DC huyo alitaka kujua nini hasa kilichowafanya watembee safari ndefu kama hiyo?

DC Rugimbana alisema, walimweleza kuwa Mosi, Wanataka Kumnuona Rais ili wamueleze kuchukizwa kwao na vitendo vya viongozi kula rushwa na hakuna hatua dhabiti zinazochukuliwa dhidi yao, kukithiri kw amatumizi mabaya ya rasilimali za taifa, kukithiri kwa vitendo vya unyanyasaji dhidi ya raia, na kudai kurejeshwa kwa serikali ya Tanganyika.

 

Baada ya kusikia hayo, DC aliwaeleza kuwa kila Mtanzania anayo haki ya kumuona Rais wa nchi, hata hivyo sio kumuona kiholela bali ni kwa utaratibu maalum, na kwa kufikia hatua waliyofikia vijana hao, tayari walikuwa wamevunja sheria lakini akawataka wasubiri awasiliane na wakubwa ili waandaliwe utaratibu wa kumuona Rais.


Hata hivyo vijana hao walikataa na walipotoka nje ya ofisi ya DC hapo Kinondoni, walifanya tena jaribio la kuelekea Ikulu na safari hii polisi hawakufanya masihara, waliwaweka chini ya ulinzi mita chache kutoka taa za kuongozea magari kwenye makutano ya barabara za Morogoro na Kawawa ukiwa uneelekea Kariakoo.

Vijana hao wakiwa kwenye safari yao eneo la Magomeni Kagera

Vijana hao wakiwa chini ya ulinzi wa polisi wakielekea kituo cha polisi Magomeni Mapipa 

Polisi wa kutuliza ghasia akiwahi sehemu walikoelekea vijana hao tayari kuwakamata

Polisi wakionye raia kutounga "tela" safari ya vijana hao wakati wakiwa eleo la Magomeni Mwembechai

Polisi wakimdhibiti mmoja w avijana wasiokubali "kupitwa"

Polisi wakiwahi kukamata vijana

Vijana wakiwa chini ya ulinzi

Wakionyesha mshikamani baada ya kukamatwa

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Jordan Rugimbana, akiwaeleza waandishi wa habari matokeo ya mazungumzo yake na vijana hao.

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO