Picha ya Makataba: Mbunge wa Arusha Mjini, Mh, Godbless Lema akihutubia wananchi katika moja ya mikutano ya chama chake Chadema Jijini Arusha.
*****
Katibu wa Chadema Jimbo la Arusha Mjini, Bw Lewis Kopwe na Katibu Mwenezi wake Bw Gabriel Kivuyo wametoa ratiba ya mikutano mfululizo ya chama hicho kwa Kata kadhaa za Jimbo la Arusha Mjini zikilenga kuwakutanisha wananchi na viongozi wapya waliowachagua kuongoza Serikali za Mitaa maeneo tofauti ya Jiji.
Ratiba hiyo ni kama ifuatavyo
No. | Tarehe | Eneo la Mkutano/Mtaa | Kata | Maelezo |
01 | 05/01/2015 | Samunge | Levolosi | Umeshafanyika |
02 | 10/01/2015 | Shuma | Elerai | |
03 | 17/01/2015 | Esso | Unga Ltd | |
04 | 24/01/2015 | FFU | Murriet | |
05 | 31/01/2015 | Soko Kuu | Kati | |
06 | 05/02/2015 | Kambi ya Fisi | Ngarenaro | |
07 | 07/02/2015 | Bluehouse | Daraja Mbili |
Aidha Katibu huyo amesema kuwa kutakuwa na mikutano ya ziada nje na ratiba hii kwa maeneo mengine kuanzia tarehe 18/01/2015 mfululizo hadi tarehe 24/01/2015 ambapo baadhi ya wabunge wa chama hicho wamealikwa na viongozi wa Kata nyingine kuzungumza na wananchi.
Mwenyekiti wa chama hicho Jimbo la Arusha Mjini, Bw Derick Magoma amethibitisha kuwa mikutano hii yote na ratiba yake kama ilivyo tayari ina baraka za Jeshi la Polisi kuhakikisha wanatoa ulinzi maeneo hayo.
Ikumbukwe kuwa katika uchaguzi ulioisha Chadema wameshinda jumla ya mitaa 76 kwa wenyeviti wa wajumbe wote na mitaa 5 wakiwa na wajumbe wote wao isipokuwa Mwenyekiti!
CCM wao wameshinda mitaa 78 ueyekiti lakini katika hiyo mitaa mitano wajumbe wote ni wa Chadema na mitaa 6 haikuwa na ushindani baada ya wagombea wa Chadema kuenguliwa. Kwa hiyo ni sawa na kusema katika mitaa ambayo wameshindana CCM imepata Mitaa 67 pekee ikiwa ni matokeo ya mbinu ovu na hila za kila namna pamoja na msaada wa wasimamizi na polisi.
CHANZO: JAMII FORUMS
0 maoni:
Post a Comment