Mbunge wa Arumeru mashariki Joshua Nassari akifanyiwa maombi na wakazi wa jimbo lake mara baada ya kutoa msaada wa mifuko ya cement kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule tatu tofauti wilayani Arumeru
Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari akisomewa kitabu cha Hadithi na Mwanafunzi wa shule ya Msingi Sura iliyopo wilaya ya Arumeru jana alipofika kutoa mchango wa mifuko 50 ya saruji katika kusaidia ukarabati wa shule hiyo.Jumla ya shule tatu za msingi Sura,Kulala na Ulonga zilikabdidhiwa mifuko 150 ya Saruji.Picha na Ferdinand Shayo.
Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua akijadiliana jambo na Viongozi wa Kamati ya Shule ya msingi Kulala mara baada ya kukabidhi mifuko 50 ya saruji ikiwa ni mchango wa Mbunge huyo katika kusaidia ukarabati wa shule hiyo.Jumla ya shule tatu za msingi Sura,Kulala na Ulonga zilikabdidhiwa mifuko 150 ya Saruji.Picha na Ferdinand Shayo.

Shule za Msingi za Sura, Kulala na Ulonga zilizopo wilaya ya Arumeru zinakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa majengo pamoja na ukosefu wa huduma za choo hali inayoathiri hali taaluma katika shule hizo.
Akizungumzia changamoto hizo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Sura Sifaeli Akiyoo amesema kuwa hali ya Taaluma shuleni hapo itaboreshwa iwapo kutakuwepo na mazingira mazuri ya Wanafunzi kujifunzia wawapo shuleni hivyo ameiomba jamii kujitokeza kusaidia shule hiyo ili iweze kufanya vizuri kitaaluma.
Mtendaji wa Kijiji cha Sura Kaanael Pallangyo amesema kuwa juhudi za wananchi na mashirika pamoja na serikali zinahitajika ili kuwajengea wanafunzi mazingira bora ya kujifunzia na ili waweze kufaulu vizuri katika masomo yao.
Kutokana na Changamoto hiyo Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari ambapo amechangia mifuko 150 ya saruji katika shule za Sura, Kulala na Ulonga ili kuwezesha ukarabati wa majengo ya shule hizo ambazo hali yake bado hairidhishi.
Nassari amewaasa Wananchi wa vijiji hivyo kuunganisha nguvu na kushirikiana na serikali ya Kijiji katika kuboresha hali ya elimu .
Sekta ya Elimu ni sekta nyeti nchini ambayo ikitiliwa mkazo inaweza kusaidia kupunguza umasikini,maradhi na ujinga ,hivyo jitihada za dhati zinahitajika ili kuifanya elimu kuwa silaha bora itakayowasaidia Vijana na Watanzania kubadilisha maisha yao na kuliletea maendeleo taifa.
Stori Na Picha: Ferdinand Shayo, Arumeru.
0 maoni:
Post a Comment