Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe Freeman A.Mbowe akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini Mhe Israel Natse wakiwa wanaingia ukumbi wa JUMUIKA
Viongozi wa kuu wa Chadema Taifa pamoja na Kanda wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kikao cha baraza la kanda ya kaskazini kuanza
Waheshimiwa wabunge wakiwa wanaimba wimbo wa Taifa
Katibu wa Kanda ya kaskazini Mhe Amani Golugwa akiwakaribisha wajumbe wa kikao cha baraza la Kanda ya Kaskazini , wajumbe wa kikao wametoka katika majimbo 33 ya kanda
Mwenyekiti wa Kanda ya kaskazini Mhe Israel Nates akitoa neno la ufunguzi kwa wajumbe na kumkaribisha Naibu katibu Mkuu Zanzibar
Naibu katibu Mkuu Zanzibar Mhe Salimu Mwalimu akiongea na Wajumbe wa baraza la uongozi wa kanda ,na kufafanua majukumu na utekelezaji wa kanda kaitika ujenzi wa chama
Mhe Freeman A.Mbowe akiwa hutubia wajumbe wa baraza la kanda pamoja na waandishi wa habari, akifafanua baadhi ya mambo ambayo yanaendendea katika nchi yetu kwa sasa, pia akiitaka tume kuwa na msimamo wa siku na tarehe ya kuanza zoezi la uandikishaji wa Wanachi kwenye daftari la kupiga kura
Mwenyekiti huyo amesema kuwa chama chao kimejipanga kuahakikisha kinahamasisha kwa nguvu zote wananchi weweze kwenda kujiandikisha katika daftari la mpiga kura
Alisemakuwa hii itaweza kumsaidia kila mwananchi kuweza kupata haki yakumchagua kiongozi bora anaemtaka katika uchaguzi mkuu ujao wa kuwachagua viongozi wakuu ambao ni rais ,wabunge na madiwani.
Alisema kuwa pamoja ya kuwa tume wamekuwa wananchelewesha kufanyika kwa zoezi hili , wao wamejipanga kikamilifu na pindi ambapo zoezi hili litatangazwa kuanza rasmi watajitaidi kwa njia yoyote kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kujiandikisha
Alisema kuwa kwa upande wa kupiga kura katiba wanaendelea na msimamo wao ambao walitangaza awali wa kutoshiriki katika mchakato wa kura ya maoni ya katiba huku akisisitiza kuwa swala la kutoshiriki katika mchakato wakura za maoni auingiliani kabisa na kuhamasisha wananchi kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura
Alimaliizia kwa kuwasihi wananchi wajitokeze kwa wingi sana pindi pale ambapo watasikia zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la kudumu limewadia ili waweze kupata haki yao ambayo itawaruhusu kuchgua kiongozi wanao wataka.
0 maoni:
Post a Comment