Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA IKULU - RAIS KIKWETE AKIWA KWENYE MKUTANO WA UMOJA WA AFRIKA (AU) MJINI ADDIS ABABA,ETHIOPIA

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipitia moja ya taarifa wakati akiwa kwenye Mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa,Ethiopia leo.Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mh. Bernard Membe.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika (kulia) wakikutana na marais wastaafu, Thabo Mbeki wa Afrika ya Kusini(Kushoto) na Joachim Chissano wa Msumbiji(wapili kushoto) wakati wa mkutano wa 24 wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika unaofanyika Addis Ababa Ethiopia leo.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Malawi Professa Peter Mutharika jijini Addis Ababa Ethiopia leo.Viongozi hao wanahudhuria mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais wa Malawi Professa Peter Mutharika(Wanne kushoto), Rais mstaafu wa Msumbiji Joachim Chissano, Rais mstaafu wa Afrika ya Kusini Thabo Mbeki(kulia) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe (kushoto)wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya kukutana wakati wa mkutano wa wakuu wan chi wanachama wa AU unaofanyika jijini Addis Ababa Ethiopia(picha na Freddy Maro)

 

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO