OPERESHENI ya kukamata
madereva wa magari wanaofanya
makosa ya barabarani,
inayoendana na utozaji wa tozo
za faini, imewaondoa Askari wa
Usalama Barabarani, kwenye
jukumu lao la msingi la
kuhakikisha usalama wa
watumiaji wa barabara, na
kuwapeleka kwenye ukusanyaji
wa mapato unaotiliwa shaka kiasi
cha kuibua maswali mengi
miongoni mwa wadau wa
barabara nchini.
Uchunguzi uliofanywa na World
over challenge kwa siku kadhaa
sasa umebaini kuwepo kwa
mbinu za askari hao wa usalama
barabarani kujificha vichakani ili
tu kukamata magari yanayokiuka
taratibu za matumizi ya barabara
kwa lengo la kujipatia fedha, hali
inayotia shaka kama fedha zote
zinazokusanywa na askari hao
zinaingia kwenye mfumo wa
mapato ya Serikali au nyingine
zinaishia mifukoni mwao.
Malalamiko ya madreva wa
magari
Baadhi ya madereva katika
maeneo mbalimbali nchini
wamelalamikia kitendo cha askari
hao kuwakamata na kuwaamrisha
kulipa faini za papo kwa hapo
badala ya kuwaelimisha wakosaji
juu ya baadhi ya mambo
wanayokosea wakiwa
barabarani. Kwa mujibu wa
madereva hao, si kila kosa
linalofnyika barabarani linatakiwa
litozwe tozo, bali yapo baadhi ya
makosa ambayo dereva
anapaswa kukamatwa na
kuelimishwa tu bila kuadhibiwa.
Wanayataja baadhi ya makosa
ambayo yanahitaji kukumbushwa
tu kwa madereva, kama sheria ya
usalama barabarani ya mwaka
2011 inavyosema kuwa ni pamoja
na dereva na abiria wake kusahau
kufunga mkanda na magari ya
kubeba abiria kutoandikwa jina
ubavuni.
Chanzo: HAPA
0 maoni:
Post a Comment