Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru) mkoani Arusha imemhoji mkurugenzi mkuu wa kituo cha zana za kilimo na teknolojia vijijini (Carmatec),Elfariji Makongoro pamoja na baadhi ya watumishi wa taasisi hiyo kutokana na sakata la ufisadi wa majengo mawili makubwa yaliyopo ndani ya taasisi hiyo.
Majengo hayo ni yale yanayotazamana mkabala na kiwanda cha kutengeneza matairi cha General Tyre cha jijini Arusha ambapo taasisi hiyo iliyafungulia zabuni mwaka jana kwa ajili ya kuyapangisha mwaka juzi lakini katika hali isiyo ya kawaida mara baada ya kutangaza kwa washindi wa zabuni hizo na malipo kufanyika mchakato huo ulisitishwa ghafla.
Hadi sasa majengo hayo yako wazi kufuatia washindi wa zabuni hizo kufungua shauri lao mahakamani wakitaka kulipwa fedha walizolipa kwa ajili ya kupangisha ndani ya majengo hayo ambazo ni zaidi ya $ 10,000 sawa na zaidi ya sh,15 milioni.
Habari na: Moses Mashalla
0 maoni:
Post a Comment