Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Wanahabari kutoka vyombo mbali mbali vya habari nchini wametembelea kituo cha watoto yatima cha Huruma Children Center kilichopo Mtaa wa Morombo na kuwafariji pamoja na kuwapeleka zawadi.
Katika Ziara hiyo iliyoandaliwa na Kampuni ya jamii media ambao ni wamiliki wa jamiiblog.co.tz ililenga kuwakutanisha Wanahabari na makundi maalumu katika jamii ikiwa ni njia ya kujitoa kwa jamii na kuwa faraja kwa waliokosa faraja.
Mkurugenzi wa Jamii media ,Pamela Mollel amesema kuwa mbali na kuripoti matukio mbali mbali yanayojiri nchini Wanahabari wana jukumu la kuisaidia jamii kwasababu wao ni sehemu ya jamii .
Pamela Mollel ameeleza kuwa suala la kujitoa kwa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu ni jukumu la kila Mtanzania ili kuwasaidia kuwa na maisha bora na kuisaidia jamii pia.
Mwandishi wa Kituo cha TV 1 Mkoani hapa Jane Edward ameeleza kuguswa na watoto hao wenye vipaji lukuki ambavyo vikiendelezwa wanaweza kuwa tunu ya taifa na kuliletea taifa ushindi katika sanaa na michezo.
“Watoto hawa licha ya kuwa yatima wana uwezo mkubwa ambao ukitumiwa vizuri unaweza kulisaidia taifa letu wengine ni wabunifu mashirika binafsi ,serikali na mtu mmoja mmoja kuwaunga mkono watoto hao” Alisema Jane Edward
Mmiliki wa blogu ya Wazalendo 25 Blog Bw. Gadiola Emmanuel anasema kuwa ni wakati sasa kwa wanahabari kuwa mfano wa kuigwa katika kuisaidia jamii na kuongoza mabadiliko wanayoyataka kuyaona badala ya kuwa wasemaji peke yake hususani katika masuala ya kijamii ushiriki wao utaleta mabadiliko chanya na ushawishi mkubwa.
Mkurugenzi wa Jamii Blog Bi. Pamela Mollel Akitoa Zawadi kwa Mmoja wa Mtoto katika kituo cha watoto yatima cha Huruma Children's Trust Centre Kwa Morombo, Jijini Arusha katika siku ya Wapendanao.
Waandishi wa Habari wa Arusha wakitoa Zawadi zao za "Valentine's day" kwa watoto wa kituo cha Huruma Children's Trust Kwa Morombo, Jijini Arusha, kama ishara ya Upendo na Kuwajali watoto yatima katika siku hii muhimu ya Wapendanao. Kushoto aliyesimama ni Mratibu wa Shughuli hiyo Bi. Jane Edward Kutoka TV1 -Arusha. Zawadi hizo zilitolewa Tarehe 14.02.2015 Jumamosi.
Wakurugenzi wa Wazalendo 25 Blog Bw. Gadiola Emanuel na Jamii Blog Bi. Pamela Mollel tukitoa zawadi kwa mmoja wa watoto wa Huruma Children's Trust Centre Kwa Morombo, Jijini Arusha. kama ishara ya Upendo katika Sherehe ya siku ya wapendanao
Mwandishi wa Habari wa Tanzania Daima Bw. Ferdinand Shayo na Mwandishi Huru na Mmiliki wa Blog ya Wazalendo 25 Blog Bw. Gadiola Emanuel Wakishusha mzigo ambao ni moja ya zawadi ya Upendo kwa Watoto yatima wa Kituo cha Huruma Children's Trust Centre, Kwa Morombo, Jijini Arusha. Tarehe 14/ 2/2015 Jumamosi.
Siku ya Wapendanao Pamoja na Watoto Yatima ...........katika kituo cha Huruma Children's Trust Centre Kwa Morombo, Jijini Arusha.
Hapa ni Bwenini la watoto wa kiume wa kituo cha watoto yatima cha Huruma Children's Trust Centre Kwa Moromboo, Jijini Arusha.
Pamela Mollel Akimlisha mtoto yatima katika kituo cha Huruma Children's Trust Centre Kwa Moromboo, Jijini Arusha.
Sema Hellooooooo........
Bi. Jane Edward wa TV1 -Arusha akimlisha mmoja wa Watoto yatima katika kituo cha Huruma Children's Trust Centre Kwa Moromboo, Jijini Arusha.
Mdau wa Habari na IT wa Palace HoteL Arusha Bw. Ricki Justin akitoa zawadi kwa mmoja wa watoto yatima wa kituo cha Huruma Children's Trust Centre Kwa Moromboo, Jijini Arusha
Ricki na Gadiola Emanuel wakikabidhi mzigo kwa mmoja wa watoto yatima wa kituo cha Huruma Children's Trust Centre Kwa Morombo, Jijini Arusha.
Mratibu wa Shughuli hii na Mwandishi wa Kituo cha Runinga cha TV1 Bi. Jane Edward akitoa moja ya zawadi kwa Matron wa kituo cha watoto yatima cha Huruma Children's Trust Centre Kwa Morombo, Jijini Arusha.
Kushoto ni Pamela Mollel wa Jamii Blog na Kulia ni Jane Edward wa TV1- Arusha wakimkabidhi Matron wa watoto yatima wa kituo cha Huruma Children's Trust Centre Kwa Morombo, Jijini Arusha.
The CEO wa Wazalendo 25 Blog Bw. Gadiola Emanuel na Mratibu Bi. Jane Edward wa TV1 -Arusha wakipata historia fupi ya kituo cha Huruma Children's Trust Centre Kwa Moromboo, Jijini Arusha.
Muonekano wa kituo cha Huruma Children's Trust Centre .
0 maoni:
Post a Comment