Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

HAKI ZA BINADAMU WAPINGA UKATILI,UNYAMA NA VITENDO VYA KUTWEZA ALIVYOFANYIWA MHITIMU MWANAJESHI WA JKT KIONGOZI WA WALIOTAKA KUANDAMANA

 

                                               clip_image002                             

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UKATILI,UNYAMA NAVITENDO VYA KUTWEZA ALIVYOFANYIWA MHITIMU MWANAJESHI WA JESHI LA KUJENGA TAIFA

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRD- Coalition) unalaani kwa nguvu zote kitendo cha kutekwa na kuteswa kwa mwenyekiti wa JKT Tanzania Bw. George Mgoba (28), pamoja na kushikiliwa kwa viongozi wengne bila dhamana.

Mtandao umesikitishwa kupokea taarifa Mnamo wiki iliyopita kuwa Bw. Mgoba alipotea gafla siku ya tarehe kumi na sita baada ya kusimamia utoaji wa tamko la kutangaza maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanywa tarehe 23 Mwezi wa Pili na wahitimu wa JKT, na baadae kupata taarifa kuwa kalazwa katika hospitali ya Tumbi baada ya kuokolewa na msamaria mwema katika mapori ya kibaha akiwa amenyolewa nywele kichwani upande mmoja kwa nia ya kumchoma sindano yenye dawa ambayo hadi sasa haijafahamika. Aidha sindano hiyo haikupitishwa kichwani kutokana na maelezo yake kuwa watesi wake walikosa mshipa na hivyo kuchoma mkononi.

Bw. George Mgoba ambaye ni mweyekiti wa Taifa wa vijana wa JKT waliokosa ajira, alikua akisimamia mchakato wa maandamano ya Amani ili lkushinikiza serikali iwawezeshe waweze kutengeneza kikosi cha ulinzi kitakacho tumika kulinda ofisi za serikali kwa bei rahisi. Vijana hao walisema kuwa sio kuwa wanaomba ajira bali wanaomba kuwezeshwa ili wajiwezeshe kwani sasa ni idadi kubwa (3000) nchi nzima walio pokea mafunzo ya kijeshi kwa muda wa miaka miwili na kutelekezwa swala ambalo linaweza hatarisha usalama wa nchi kama baadhi yao wakijiingiza kwenye makundi yasiyofaa.

Katika tafiti zake Mtandao umegundua kuwa Bw. Mgoba alipokea simu mnamo saa tano asubuhi akiwa nyumbani kwake mabibo Loyola huku mtu aliyejitambulisha kama kijana mwenzie wa JKT akimuambia wakutane Mabibo mwisho ili ampatie copy za vyeti vyake vya JKT, alieleza mkewe. Ila baada ya hapo simu yake haikupatikana tena. kumbe tayari alikuwa kesha tekwa na wanawake wawili pamoja na mwanaume mmoja (watesi walibadilishana zamu mara tatu) hivyo watu wengine kuingia na kumpeleka eneo la mateso ambalo yeye alisema ni kama walikua wanaingia ndani ya shimo. Baada ya kupigwa sana walimuhamishia katika pori wa kibaha ambapo alijikongoja mpaka pale alipookotwa na msamaria mwema.

Baada ya kuokotwa na msamaria ambaye alimpeleka Bw. Mgomba katika kituo cha polisi Tumbi na baada ya hapo hospitali ya Tumbi ambapo aliwekewa drip maji na hakupewa matibabu yoyote. Kutokana na viashiria kuwa Bw. Mgomba angeweza kuwa kachomwa sindano yenye madhara au sumu familia iliomba ruhusa kumchukua mgonjwa kutoka Hospitali ya Tumbi kibaga na kwenda hospitali binafsi lakini walinyimwa ruhusa katika ofisi ya RPC polisi Kibaha kutokana na polisi kusema kuwa ni jukumu lao kumuhamisha na kumpeleka Muhimbili hospital jambo ambalo halikuwa la kweli kwani baada ya hapo walimpeleka Central police Dar es Salaam na kisha kumpatia nauli ya elfu mbili ili arudi kwake bila kujali maumivu aliyokuwa nayo.

Mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu pamoja na timu ya Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu walipofika katika hospitali ya Amana ili kuweza kupata habari juu ya Muhusika, ushirikiano haukua mzuri kwani ilionyesha kuwa mgonjwa alikua katika ulinzi Mkali.

Ikumbukwe kuwa, matukio ya hivyo kwa watetezi wa haki za binadamu, hasa viongozi wa makundi ya maandamano au wadai haki hayajaanza leo, Mfano hai ni ule wa Alfajiri ya tarehe 27 Juni 2012, tulipata taarifa kuwa Dkt. Ulimboka ambaye mwanzoni alikua amepotea alipatikana na alikua ameshikiliwa katika kituo kidogo cha polisi huko Bunju.Tuliambiwa kuwa Dkt.Ulimboka alipatikana akiwa amepoteza fahamu na kuokotwa na msamaria mwema katika msitu wa Mabwepande jijini Dar-es-salaam na alikua ametokwa na damu nyingi sana. Waliomuokota ndio waliompeleka katika Kituo cha polisi Bunju.

Kutokana na Unyama huu Mtandao wa watetezi wa haki za Binadamu kwa niaba ya Asasi washirika na Watetezi wa Haki za Binadamu nchini pamoja na kwa dhati tunalaani vikali kitendo cha kumtesa Mtu wa aina yoyote hasa pale anaposimamia haki zake na za watu wengine.

Wito wetu,

a) Kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

i. Kwanza serikali itoe matibabu yanayofaa kuokoa maisha ya George Mgoba

ii. Kufanya uchunguzi wa dhati wa tukio hili zima ;

iii. Kuwawajibisha wale wote waliohusika na tukio hili na wakala wao na kulitaarifu Taifa kuhusu watu hao na sababu za kufanya jambo hili ovu lililomletea madhara Bw. George;

iv. Na kwa weledimkubwa kuwatia hatiani na kuwashtaki wote waliohusika

v. Na kuhakikisha wahusika hao wanapata adhabu kali watakapotiwa hatiani.

vi. Tunaishauri serikali iwasikilize wahitimu wa JKT ili kuweza kutambua kama hitaji lao linatekelezeka kwani hawaombi ajira bali wanaomba fursa ya kuwezeshwa ili kuweza kujiajiri kutokana na kuwa wengi wao wanatokea katika familia duni jambo linalofanya mipango yao ikwame.

b) Kwa Jeshi la Polisi:

- Kuacha kuwa na upande wowote katika mgogoro unaoendelea kati ya madaktari na serikali;

- Kuheshimu utawala wa sheria, haki za binadamu, kutomchukulia mtu kama ana hatia kabla haijathibitishwa na kuwa na weledi katika yote wanayoyatenda;

- Kuacha kutumia mabavu na uonevu pale watu wanaposimama kutetea haki zao

c) Kwa watetezi wa haki za Binadamu:

- Kusimama Imara na kuendelea kutetea haki bila kuogopeshwa na vitendo kama hivi

- Kuungana kwa pamoja na kuwa na sauti moja ya kulaani uonevu na unyanyasaji wa watetezi wa haki

d) Kwa Wataalamu wa Tiba:

- Kutoa huduma husika kulingana na hali ya mgonjwa ili kuokoa maisha yake upesi,. Hii ni sababu hata siku ya pili toka mgojwa ahamishwe hospitali tatu yani Tumbi, Mnazi mmoja na Amana mgonjwa alikua hajapokea matibabu ya aina yoyote sababu kuwa hana PF3.

e) Kwa Wananchi /umma wa watanzania,

- Kuunga mkono shughuli zote zinazofanyika katika kutafuta haki zinazohusiana na tukio hili

- Kudai uwajibikaji na maboresho ya huduma za kijamii hasa hasa huduma za afya Tanzania.

- Kulaani vitendo vyote kama hivi vinavyokiuka haki za binadamu.

Itambulike kuwa, lililotendeka ni kosa la jinai, na kama ni tendo lililofanywa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania basi ni vyema kufahamu kuwa nchi hii inaelekea mahali pabaya. Kitendo hiki kimefanywa kwa kukusudia na havitakiwi kuendelea kutendeka katika nchi ya kidemokrasia kama hii.

Imetolewa tarehe 22/Feb/2015

………………………….

Mratibu wa Mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu

Bw. Onesmo Olengurumwa

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO