Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MULTICHOICE YAZINDUA KING’AMUZI KIPYA CHA DStv HD

unnamed

Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi (Katikati) akifafanua jambo kwenye mkutano na wanahabari  (hawapo pichani), wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa king'amuziki kipya cha  DStv HD  leo jijini Dar. Kulia ni kwake ni Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo na kushoto ni Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog)

Na Andrew Chale

KAMPUNI ya MultiChoice Tanzania wasambazaji wa ving’amuzi vya DStv, leo imezindua king’amuzi kipya cha DStv HD ambacho kitaanza kutumika kwa mara ya kwanza hapa Nchini.

Akizungumza  na wandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam,  Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania, Ronald Shelukindo, akielezea umuhimu wa huduma hizo alisema king’amuzi hicho kina ubora wa hali ya juu ikiwemo kuonyesha picha zenye ubora mzuri zaidi.

Pia alieleza kuwa, DStv HD mteja atapata kuona picha zenye mvuto zaidi pamoja na kiwango cha juu cha sauti Dolby Digital 5.1.

“Wateja wa DStv watafurahia ving’amuzi hivi kwa ubora wa hali ya juu  hivyo ni wakati wa kuchangamkia  ofa kwani ndio mara ya kwanza kuingia kwa Tanzania” alisema Ronald Shelukindo.

DSC_0239

Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akielezea ubora wa king'amuzi hicho cha DStv HD wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari leo jijini Dar.

Ronald Shelukindo akielezea kwa kina, alisema DStv HD, mteja anaweza kufurahia vipindi mbalimbali ikiwemo mifumo na mipangilio ya kila vipindi kwa kupendekeza atazame kipi gani, muda gani na wakati gani?.

King’amuzi cha “DStv HD, mteja anaweza kujipangia atazame kipindi gani ama kwa wakati autakao yeye, ambapo anachoweza ni kuseti hicho kipindi akipendacho na kisha anaweza kukiangalia kwa wakati wake, hata kama muda umepita kwa wakati huo kinarushwa kwenye chaneli husika” alifafanua Ronald Shelukindo.

Kwa upande wake,  Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu  aliwahimiza watanzania kuchangamkia vinga’muzi hivyo vya DStv HD, ambavyo kwa sasa vipo karibu maduka yote ya Mawakala wa  DStv,  kwa bei rahisi kabisa vikiwa vinapatikana kwa sh 99,000/ kwa mteja mpya huku kwa wateja walio na ving’amuzi vya zamani vya DStv watakaotaka kubadilishiwa, watalipia sh  39,000/ tu.

DSC_0140

Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akionesha king'amuzi kipya cha DStv HD kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).

“Ofa hii ni kwa ajili ya kipindi hiki cha fainali za AFCON, hadi hapo michuano hii itakapofikia tamati ambapo  bei itabadilika kutoka hizi za sasa, hivyo ni wakati wa kuchangamkia ofa hii ya kipekee na kwa mara  ya kwanza, kupata kitu cha ubora wa hali ya juu na kwa bei rahisi.” Alisema Furaha Samalu.

Kwa upande wake, Afisa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi alieleza kuwa,  siku zote MultiChoice itaendelea kuwa mstari wa mbele kwa kutoa huduma zilizo bora na za kisasa katika ulimwengu huu wa digitali ambapo bidhaa hizo za DStv zimeendelea kuwa bora kila siku.

“Huduma za DStv  siku zote zimekuwa bora ikiwemo kutoa huduma zisizoleta usumbufu.  Ving’amuzi vyetu daima vinaonyesha ubora wa hali ya juu na hutoweza kusumbuliwa na ukatikaji wa picha ama mikwaruzo... Hivyo ni wakati sasa wa kuchangamkia ofa hizi.” Alibainisha Barbara Kambogi.

DSC_0194

Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu akifafanua bei za king'amuzi hicho kipya ambapo kwa wateja wapya watajipatia kwa ofa ya Tsh. 99,000/  kuanzia leo hadi siku Jumapili kilele cha fainali za michuano ya AFCON huku ambao ni wateja tayari wanabadilishiwa kwa gharama ya Tshs. 39,000/  ambayo pia ni ofa. Ving'amuzi hivyo vipya vya DStv HD vinapatikana kupitia mawakala wote wa DStv Tanzania nzima.

Katika hatua nyingine, DStv  wamezindua huduma mpya  kwa wateja wao waliounganishwa na ving’amuzi hivyo vya DStv  kuweza kuendelea kufurahia huduma hiyo kupitia simu zao za viganjani zenye uwezo wa ‘Android’,  Kompyuta mpakato (Laptop), Tablet,  na vifaa vingine vyenye uwezo wa kupokea usajili wa ‘App’.

Akielezea, juu ya huduma hiyo,  Ronald Shelukindo, alibainisha kuwa, kinachotakiwa ni kwa mteja wa DStv, kwenda kwenye simu yake au Laptop, ama  Tablet na kisha kujisajili kupitia ‘App’   kwa kujisajili kwa kuandika  ‘DStv Now’.

Aidha, Ronald  Shelukindo alisisitiza kuwa, huduma hiyo ya  DStv Now  ni kwa wateja waliouganishwa na ving’amuzi hivyo tu ambapo wataifurahia huduma hiyo kwa kuendelea kuangalia chaneli zaidi ya 12 za DStv, ikiwemo ya Super Sport 3, za filamu, na nyinginezo mbalimbali.

Pia  kwa maelezo zaidi wateja wanaweza kutembelea tovuti  ya DStv.com

DSC_0209

Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akionesha huduma mpya ya DStv Now ambayo mteja ataweza kuangalia vipindi vya DStv kupitia simu yake ya kiganjani, kompyuta mpakato (Laptop) pamoja na Tablet. Huduma hii ni kwa wateja ambao wameunganishwa na ving'amuzi vya DStv kupitia akaunti zao.

DSC_0225

Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi (katikati), Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo (kulia) na Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu (kushoto) wakiangalia promo ya namna ya kujiunga na huduma ya DStv Now "application" inayopatikana katika simu zote za Android pamoja na kompyuta mpakato (Laptop)  unajiunga kwa kutembelea www.dstv.com

DSC_0228

Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar leo.

DSC_0247

Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo (katikati) na Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu (kulia) na Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi (kushoto) wakipozi na king'amuzi kipya cha DStv HD.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO