Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA: ZIARA YA RAIS KIKWETE MKOANI KILIMANJARO NA KUZINDUA JENGO KUBWA LA NSSF

KJ4

KJ3 KJ4

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Waziri wa Kazi na ajira Mh.Gaudensia Kabaka(watano kushoto) Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt.Ramadhani Dau(wapili kulia), Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama(wapili kushoto) pamoja na viongozi na wadau wengine wakikata utepe kufungua rasmi jengo la kitega uchumi la NSSF Kilimanjaro Commercial Complex mjini Moshi,Mkoani Kilimanjaro jana. KJ5

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt.Ramadhan Dau pamoja na wadau wengine wakitazama ramani ya jengo jipya la kitega uchumi la NSSF mjini Moshi Kilimanjaro Commercial Complex wakati wa hafla ya ufunguzi jana. KJ6

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na chipikizi wa Tanzania Girl Guides wakati wa hafla ya ufunguzi wa jengo la kitega uchumi la NSSF mjini Moshi jana.Tanzania Girl Guides,UMATI,Tanzania Red Cross ni wadau wa NSSF katika mradi huo. KJ7

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt.Ramadhani Dau baada ya hafla ya ufunguzi wa jengo jipya la kitega uchumi la NSSF mjini Moshi jana.Katikati ni Waziri wa Kazi na Ajira Mh.Gaudensia Kabaka

KJ1

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua jengo la upasuaji katika hospitali ya rufaa ya Mawenzi mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro muda mfupi baada ya kulifungua jana.Kulia ni Naibu Waziri wa Afya Dkt.Steven Kebwe. KJ2

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wauguzi wa hospitali ya rufaa ya Mawenzi mjini Moshi muda mfupi baada ya kufungua jengo la upasuaji na kuweka jiwe la msingi kuzindua ujenzi wa wodi ya mama na watoto katika hospitali hiyo jana.(wanne kulia ni Naibu waziri wa Afya Dkt.Steven Kebwe,wanne kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama,Kushoto ni Mbunge wa Vunjo Agustino Lyatonga Mrema,na wapili kushoto ni Mbunge wa Moshi Vijijini Dkt.Cyril Chami.

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO