Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

CHADEMA waunguruma Namanga na kuhimiza Wanachi Kujiandikisha; Mjumbe Halmashauri Kuu CCM Arusha Ahamia Chadema

IMG-20150221-WA0092Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha Mh Amani Golugwa akihutubia wananchi wa Namanga Wilaya ni Longido jana baada ya kumpokea aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Arusha ambaye alihamia rasmi Chadema na kupokelwa katika kikao cha ndani kabla ya mkutano huo wa hadhara.

IMG-20150221-WA0104

Mbunge wa Viti Maalumu CHADEMA, Mh Cecilia Paresso akizungumza na wananchi wa Namanga Wilayani Longido wakati wa Mkutano wa hadhara wa chama chake Wilayani humo kushukuru wananchi kuichagua Chadema katika uchaguzi wa vitongoji na Mitaa mwishoni mwa mwaka jana ambpo pia walitumia nafasi hiyo kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura wakati zamu yao itakapofika.

IMG-20150221-WA0084

Kutoka kushoto; Diwani wa Kata ya Levolosi Mh Ephata Nanyaro Mbunge Viti Maalumu Arusha Mh Joyce Mukya wote wa CHADEMA na Mwandishi wa Tanzania Daima Ausha Bi Grace Macha wakifuatilia jambo katika kikao cha ndani kabla ya mkutano wa hadhara wa shukrani baada ya Wilaya ya Longido kuchagua viongozi wengi wa Vijiji na Vitongoji watokanao na Chadema. Wilaya hii ya Longido ndio iliyochagua viongozi wao wengi kupitia Chadema kuliko Wilaya nyingine zenye wakaazi wengi jamii ya Maasai.

IMG-20150221-WA0085

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini Bw Amani Golugwa (katikati)akimpokea kamanda mpya kutoka Longido, Bw Francis Ikayo ambaye alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Kamati ya Siasa Mkoa wa Arusha. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Arumeru Magharibi Bw Gibson Meseiyaki ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Olturoto kupitia CHADEMA.
Bw Thomas ameeleza sababu za kujiengua kwake kutoka CCM na kujiunga Chadema kuwa ni msukumo aliokuwa nao kwa miaka mingi kuona mabadiliko ya kiuchumi na kijamii Wilayani Londigo. Akifafanua zaidi anasema ameamua kujiunga Chadema kwasababu Longido kuna changamoto nyingi ikiwemo ya ardhi ya malisho, makazi, kilimo, maji n.k ambapo imefikia hadi wananchi kuchomewa nyumba zao na CCM imeshindwa kuitatua na hivyo kuja kwake Chadema atapata jukwaa la kuwasemea wananchi wa Longido tofauti na akiwa CCM ambako sio rahisi kupata jukwaa la kuwasemea walalahoi.

IMG-20150221-WA0090

IMG-20150221-WA0089

Diwani wa Levolosi, Ephata Nanyaro (kushoto) akifuatilia kwa karibu yanayoendelea kweye kikao cha ndani

IMG-20150221-WA0096

Wananchi wa Longido eneo la Namanga wakiwa wamejipanga barababrani kuulaki  msafara wa viongozi wa Chadema waliokuwa wageni maalumu kwa mkutano wa shukrani baada ya Chadema kushinda vijiji na vitongoji katika uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana. Katika Mkutano huo viongozi mbalimbali wa chama na wabunge na madiwani wa chama hicho walishiriki kwa pamoja miongoni mwao akiwemo Mwenyekiti Chadema Arusha Amani Golugwa, Diwani Ephata Nanyaro, Diwani Gibson Meseiyaki, Wabunge Viti Maalumu Cecilia Paresso na Joyce Mukya, Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari na James Ole Millya mtia nia Simanjiro

IMG-20150221-WA0102
Kamanda wa CHADEMA anayetazamia kupambana na Ole Sendeka Jimbo la Simanjiro, Kamanda James Ole Millya akizungumza na wananchi wa Namanga jana

IMG-20150221-WA0103

IMG-20150221-WA0094

Joshua Nassari na viongozi wengine wa CHADEMA katika picha ya pamoja na viongozi wa kimila wa jamii ya Maasai waishio Wilayani Longido

PICHA ZOTE NA YEGELLA

*************************
GRACE MACHA ANARIPOTI ZAIDI: KIGOGO WA CCM ARUSHA AJIUNGA CHADEMA

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Kamati ya Siasa Mkoa wa Arusha, Francis Ikayo, amejiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Mwanasiasa huyo aliyekuwa mmoja wa wana CCM waliowania uteuzi wa kuwania ubunge Jimbo la Longido mwaka 2010 na kuangushwa na Mbunge wa sasa Lekelu Laizer, alijiunga Chadema jana, akitaja sababu kuu tatu zilizomfanya kuchukua uamuzi huo.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Namanga, mpakani mwa Kenya na Tanzania, muda mfupi baada ya kukabidhiwa kadi ya Chadema na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, Ikayo alisema amevutiwa na mikakati ya chama hicho ya kutetea haki za wanyonge.

“Nina sababu kuu tatu za kuhamia Chadema. Mosi ni kwa sababu chama hiki kimejipambanua kuwa watetezi wa wanyonge, pili kuna uhuru na demokrasia ya kila mtu mwenye uwezo kugombea bila kuwekewa mizengwe na tatu kinapiga vita rushwa, ufisadi na matumizi mabaya ya mali na fedha za umma,” alisema Ikayo.
Wazee watatu kutoka jamii ya wafugaji wa Kimasai anakotoka Ikayo, Lekishoo Loodo, Moi Lesingo na Laidinga Nangoro, walimkabidhi rungu na usinga mwanachama huyo mpya wa Chadema, ikiwa ni ishara ya kukabidhiwa majukumu ya Kiuongozi.

Akihutubia mkutano huo, Ikayo aliitaka jamii ya wafugaji kuamka na kuacha kuwa mtaji wa ushindi wa CCM nyakati za uchaguzi, kwa kile alichoeleza chama hicho kimewatelekeza kwa kuruhusu maeneo ya malisho kuvamiwa, huku wafugaji wakilazimika kuhangaika na mifugo yao kutafuta malisho.

Kwa upande wake, Lema aliwataka watu wote wenye umri na sifa za kujiandikisha kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye Daftari la Wapiga Kura, ili kupata fursa ya kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu baadaye mwaka huu.

Kwa upande wake, Mbunge wa Arumeru Magharibi, Jashua Nassari aliwaomba wachungaji, maaskofu na masheikh kote nchini, kuacha kupokea fedha haramu zinazotokana na wizi wa fedha na mali za umma zinazotolewa makanisani na misikitini na wasaka madaraka.

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO