Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Chadema "yawapiga stop" wanaowania kuwang'oa Lema na Nassari

Arusha.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(chadema), mkoa wa Arusha “kimewapiga
stop” wanachama wake, kutangaza nia ya
kugombea ubunge katika majimbo matatu,
yanayoshikiliwa na wabunge wa chama
hicho,hadi hapo Bunge litakapovunjwa rasmi
julai 2 mwaka huu.
Majimbo hayo ni jimbo la Arusha mjini,
mbunge wake, Godbless Lema, Jimbo la
Arumeru Mashariki, mbunge Joshua Nassari
na Jimbo la Karatu mbunge, Mchungaji Israel
Natse ambapo tayari kuna wanachama wa
chama hicho, wameanza kutangaza nia za
kuwang’oa wabunge hao.
Akizungumza na mwananchi leo, Katibu wa
Chadema mkoa wa Arusha, Calist Lazaro
alisema, maagizo anayoyatoa ni kutekeleza
utaratibu ambao umetolewa na Kamati Kuu ya
chama hicho,kuhusiana na uchaguzi mkuu
ujao.
“Naomba hapa ieleweke kuwa hatuzuwii mtu
kugombea lakini tunataka afuate taratibu ili
kuzuia vurugu na kama mtu akikiuka sasa
ina maana atakuwa amepoteza sifa”alisema
Lazaro.
Lazaro alisema nia ya agizo hilo ni kuondoa
vurugu na mpasuko ndani ya chama kabla ya
wakati muafaka wa kutangaza nia na kuanza
kampeni haujafika, lakini kwa majimbo yaliyo
na wabunge wa CCM, wagombea
wanaruhusiwa kutangaza nia.
Alisema chama hicho, kitatoa ratiba ya
uchaguzi karibuni na fomu za kugombea
nafasi mbali mbali zitapatikana katika ofisi za
chama hicho, katika ngazi zote ila kwa
maeneo yenye wabunge na madiwani wa
chadema, fomu zitapokelewa bila kutangaza
nia na kuanza kampeni.

http://mobile.mwananchi.co.tz/Habari/Chadema-yawapiga-stop/-/1597580/2626798/-/format/xhtml/-/t9q866z/-/index.html

Washirikishe Google Plus

About Ujenzi Connekt

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO