Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Jeshi la Polisi Arusha ndani ya kashfa nzito

LiberatusSabas

JESHI la Polisi mkoani Arusha limeingia katika
kashfa kubwa baada ya askari wake wawili
kuhusishwa na tuhuma za kushiriki vitendo vya
ujambazi na uporaji wa kutumia silaha; huku
mmoja wa askari hao akitoweka na redio ya
mawasiliano (redio call) pamoja na bunduki aina
ya SMG.
Askari hao wanaodaiwa kushikri vitendo hivyo
wametajwa kuwa ni PC Frank “Kacha” na PC
Mvanga Balele ambao wote ni askari wa
upelelezi kutoka Kituo Kikuu cha Polisi cha mjini
Arusha.
Tayari PC Frank ametiwa mbaroni mkoani
Kilimanjaro alikokwenda kupata matibabu baada
ya kujeruhiwa na polisi wa doria katika
mapambano ya kurushiana risasi na yuko katika
mahabusu ya Kituo Kikuu cha Kati kwa
mahojiano zaidi kabla ya kuchukuliwa kwa hatua
za kisheria.
Habari za zilizofikia Raia Mwema mwishoni mwa
wiki na baadaye kuthibitishwa na kamanda wa
polisi mkoani Arusha Basilio Matei zilieleza kuwa
askari hao wawili wanadaiwa kushikiriki katika
tukio la uporaji wa fedha katika duka la kuuza
vifaa vya ujenzi la Kitonga katika eneo la Njiro
Januari 15 mwaka huu.
Tukio hilo limekuja huku kukiwa na tetesi na
malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wananchi
kuwa baadhi ya askari polisi  katika mkoa wa
Arusha wanashiriki katika uhalifu hasa wa
kutumia silaha kinyume kabisa na malengo ya
Jeshi hilo na kabla ya kugundulika kwa askari
hao wawili wanadaiwa kushiriki katika matukio
mengi.
Aidha, malalamiko hayo ni pamoja na askari hao
pia kushirikiana na majambazi sugu kwa kutoa
taarifa mbalimbali za utendaji wa kazi za polisi
na hatua zinazochukuliwa polisi wakati wa
misako; huku wakipokea mgao unaotokana na
shughuli za uhalifu.
Taarifa za kiintelejensia kutoka ndani ya jeshi hilo
zilizofikia Raia Mwema zilieleza kuwa
kumekuwepo na mtandao wa muda mrefu wa
uhalifu ndani ya polisi  ambao umehusisha hata
maafisa wenye vyeo vya juu ndani ya jeshi hilo
katika matukio kadhaa ya uporaji wa kiasi
kikubwa cha fedha.
Baadhi ya matukio ambayo mtandao wa uhalifu
ndani ya jeshi hilo unadaiwa kushiriki ni pamoja
na uporaji wa fedha katika mabenki kadhaa
nchini katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
Ni mtandao huo ndiyo unaodaiwa kuwa kiini cha
uhalifu wa kutisha mkoani Arusha ambapo
takwimu zisizo rasmi zinaonyesha kuwa ndiyo mji
wa pili kwa matukio ya uhalifu na mauaji katika
eneo la Afrika Mashariki ukitanguliwa na mji wa
Nairobi ambao ni mji mkuu wa Kenya.
Akizungumza na Raia Mwema mmoja wa askari
wa upelelezi mkoani Arusha alieleza kuwa
madai kuwa kuna mtandao wa uhalifu ndani ya
Jeshi hilo ni ya muda mrefu, na hata viongozi wa
juu wa jeshi hilo nchini wanaufahamu mtandao
huo; lakini wameshindwa kuchukua hatua za
kinidhamu kwa maaskari hao kwani wengine ni
maafisa wakubwa.
“Polisi wamekuwa wakishiriki uhalifu kwa njia kuu
mbili ambazo ni kushiriki moja kwa moja katika
matukio na njia ya pili ni kushirikiana na wahalifu
kwa kuwapa taarifa za kipolisi na kuwaepusha
wasikamatwe na wao kupewa malipo
yanayotokana na shughuli za uhalifu”alieleza
askari huyo.
Askari huyo anaongeza kuwa sababu kubwa ya
polisi kugeukia uhalifu ni pamoja askari kuishi
uraiani badala ya kwenye nyumba au kambi za
kipolisi, mazingira duni ya kufanyia kazi na
uwiano usio sawa wa mishahara kati ya
maaskari wadogo na maafisa wa juu , na tamaa
inayotokana na maisha ya kifahari ya baadhi ya
maafisa; huku askari wa kawaida wakiwa katika
hali mbaya.
“Askari wanaoishi uraiani wakiona maisha ya
kifahari ya baadhi ya wana jamii wanaoishi nao
hupata vishawishi na matokeo yake hujiingiza
katika vitendo visivyofaa ili waweze kumiliki vitu
vya kifahari  kama magari, nyumba na vifaa vya
ndani”, alsema askari huyo.
“Askari wengi wanafanya kazi katika mazingira
magumu kwa mfano hatuna hata filimbi, viatu, na
silaha hutolewa kwa wanaoenda lindo katika
maeneo muhimu kama mabenki na nk…..mambo
hayo yote yamechangia sana askari polisi
kushindwa kuwajibika ipasavyo na baadhi
kujiunga na mitandao ya kihalifu”, alisema.
Kwa mujibu wa askari huyo, tatizo lingine ni
muundo mbovu wa jeshi la polisi, kushamiri kwa
upendeleo ambapo baadhi ya maafisa
wamepewa vyeo  huku wakiwa na uwezo mdogo
katika kutekeleza majukumu yao mfano ukiwa
katika kusaili wanafunzi wanaotaka kuingia katika
chuo cha polisi.
“Polisi sasa ianzishe utaratibu wa kuchukua
vijana waliomaliza mafunzo JKT badala ya
kutegemea wale ambao wamemaliza elimu ya
kidato cha nne na sita ambao wengi huwa
wamefeli mitihani ya kumaliza shule na wengine
wamefoji vyeti….na matokeo yake ni jeshi kukosa
watu wenye kujiamini na wenye akili ya
kusimamia kazi zao”, alisema.
Katika tukio la wiki iliyopita, kwa mujibu wa watu
waliolishuhudia tukio hilo, majira ya saa nane za
mchana, askari hao walikuwa miongoni mwa
kundi la majambazi waliovamia duka hilo lakini
polisi doria wapatao sita walipata taarifa
mapema na kwenda eneo hilo haraka.
Imeelezwa kuwa baada ya kufika eneo hilo, polisi
walianza kurushiana risasi na majambazi hayo
ambapo mmoja wao alijaribu kutoroka kwa
kutumia pikipiki yenye namba za usajili T 133
BAB, lakini katika harakati hizo aliteleza na
kuangukia ndani ya mtaro na ndipo polisi
walipompiga risasi ya kiuno.
Mtuhumiwa huyo, ambaye alifariki dunia muda
mfupi baadaye, alitajwa kuwa ni Hilary Kibauli
(24) mkazi wa Singida ambaye pia imeelezwa
kuwa ni mtoto wa mmoja wa maafisa wa Idara
ya Usalama wa Taifa wa cheo cha juu mkoani
humo.
Katika harakati hizo za kupambana na
majambazi, askari hao waliweza kuwatambua
wenzao wawili ambao walikuwa wamejihami na
silaha na wakati askari hao wakiwa bado
wamepigwa na butwaa wasiamini
walichokishuhudia, watuhumiwa hao waliondoka
eneo hilo kwa kuteka basi dogo lililokuwa
limewabeba wanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya
Mtakatifu Costantine lenye namba T 986 AEM.
Baada ya kufanikiwa kutoroka katika eneo hilo,
mtuhumiwa PC Balele inadaiwa kuwa alipigiwa
simu na wenzake walioko katika mtandao wa
uhalifu kwa kumweleza kuwa tayari alikuwa
ameshagundulika, hivyo kumtaka atoroke haraka
ili kusalimisha maisha yake.
Inadaiwa kuwa askari huyo alikwenda nyumbani
kwake katika eneo la Kijenge Juu na kumchukua
mke wake na vitu vichache na kutoweka
akitumia gari aina ya Toyota Prado.
Muda mfupi baadaye askari wa doria waliwasili
na kuizingira nyumba hiyo ambapo baada ya
kufanya upekuzi walifanikiwa kukuta kiasi
kikubwa cha fedha zikiwa ndani ya boksi pamoja
na vifaa mbalimbali vya kufanyia uhalifu
vikiwemo vya kufichia sura (masks).
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi
mkoani Arusha, Basilio Matei alithibitisha askari
hao kutoweka kazini tangu siku ya tukio hilo.
Askari hao pia wametajwa na marehemu Kibauli
kabla ya kufikwa na mauti kuwa alikuwa
anashirikiana nao katika uhalifu.
“Mtuhumiwa Hilary alimtaja kwa jina la PC Frank
kwa jina la  “Kacha” kuwa alikuwa anashirikiana
naye lakini bado tunamhoji na ili kupata taarifa
zaidi…..lakini kuna uwezekano kuwa alikuwa
anashirikiana na wahalifu”, alisema Matei.
Kuhusu PC Mvanga Balele, Kamanda huyo
alieleza kuwa bado hawajathibitisha kama askari
huyo alikuwemo katika kundi la majambazi
waliokuwa wamevamia duka hilo la vifaa vya
ujenzi ingawa hadi jana alikuwa ametoweka
nyumbani kwake.
“Askari waliokuwepo katika operesheni hiyo
wanadai kuwa walimwona mtu kama yeye, lakini
ni vigumu kuthibitisha lakini sisi tunajiuliza
kwanini askari huyo ametoweka nyumbani kwake
pamoja na familia yake”?.....tumepekua nyumba
na tumekuta ameacha kila kitu”, alisema Matei.
Matei pia alikanusha madai yanayotolewa kuwa
askari huyo ametoweka akiwa na redio ya
mawasiliano na bunduki yenye risasi ni ya
uwongo; kwani siku ya tukio Mvanga alikuwa
amepangiwa zamu ya lindo katika mitambo ya
Televisheni ya Taifa (TBC) na kuongeza kuwa
askari wanaokwenda doria za mchana hawapewi
silaha.
“Askari wanaopewa silaha ni wale tu
wanaokwenda doria na lindo za  usiku, lakini
mchana hatutoi silaha na redio inayodaiwa kuwa
iko mikononi mwa askari huyo si ya kweli kwani
redio hiyo ilishapatikana”, alisema Matei.
Kamanda huyo alisema kuwa kwa sasa
wameanzisha msako wa kumsaka askari huyo
kwa kuondoka kazini bila kutoa taarifa kama
taratibu za jeshi hilo linavyoeleza na kuwataka
wananchi wanaomfahamu kushirikiana na jeshi
hilo kwa  kutoa taarifa zake.
Tukio hilo la aina yake la askari kuhusishwa na
matukio ya uhalifu limevuta hisia za watu wengi
mjini Arusha  ambapo kumekuwa na malalamiko
ya muda mrefu kuwa baadhi ya askari polisi
wanashirikiana na wahalifu; hali inayofanya mji
wa Arusha kuwa mkoa wa kwanza kuwa na
kiwango cha juu cha uhalifu hapa nchini.

Chanzo: Raia Mwema 27 Jan 2015

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO