Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Kingunge jukwaa moja na Ukawa Arusha, asema CCM imeishiwa pumzi

By Sauli Giliard, Arusha.

KINGUNGE PICHA

Mwanasiasa mkongwe na miongoni wa waasisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kingunge Ngombale Mwiru leo amehutubia katika jukwaa la kampeni za Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na kusema chama tawala kimeishiwa pumzi.

Katika mkutano wa kumnadi mgombea urais kwa tiketi ya Chadema na Ukawa, Edward Lowassa katika viwanja vya Sinoni, mkoani Arusha, Kingunge amesema wale wote wanaohoji uamuzi wake wa kuihama CCM atawajibu hivi karibuni.

Huku akijinadi kuwa ni mwanabadiliko tangu kuasisiwa kwa CCM, mwanasiasa huyo mkongwe nchini amesema sababu zinazoonyesha kuwa chama tawala kimeishiwa pumzi ni kudorora kwa uchumi ambao kwa sasa unakuwa chini ya asilimia saba.

“Hivi karibuni hasa awamu hii ya sasa kuna dalili kuwa baada ya CCM kukaa madarakani kwa nusu karne sasa imeanza kuishiwa pumzi. Rais Kikwete amerithi uchumi ukiwa unakuwa kwa asilimia saba…sasa kwa mujibu wa serikali yenyewe unakuwa kwa chini ya asilimia saba. Uchumi sasa unadorora.”

Baada ya kushuka jukwaani, mgombea urais Edward Lowassa alipanda jukwaani na kuwataka wananchi wasichelewe kumpa kura ili akashughulikie matatizo yanayowakabili ikiwemo afya, elimu, kuboresha mazingira ya biashara na kukuza kipato cha wananchi.

Lowassa amesema atahakikisha Tanzania inaendesha kilimo cha umwagiliaji na kutoa uhuru kwa wakulima kuuza mazao yote kokote atapopenda tofauti na hali ilivyo sasa.

OTH_4859

OTH_4933

OTH_4991

OTH_4707
SOURCE: MWANANCHI PICHA: OTHMAN MICHUZI

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO