Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MAPOKEZI YA LOWASSA JIJINI MBEYA NI SHEEDAAAA

 

Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, amepata mapokezi makubwa mithili ya mfalme na wakazi wa jiji la Mbeya huku baadhi ya wananchi walionekana wakifagia na kudeki barabara, wakati akiwa njiani kuelekea eneo la Uwanja wa Rwanda Nzovwe, kulikofanyika Mkutano wa hadhara wa Kampeni zake anazoendelea nazo kwa nchi nzima na hii ikiwa hatua ya lala salama.

Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Mh. Joseph Mbilinyi "Sugu", wakiwasili katika uwanja wa Rwanda Nzovwe kwa Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika Jijini Mbeya leo Oktoba 18, 2015.

Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Mbeya katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe, Jijini Mbeya leo Oktoba 18, 2015.

Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akimsikiliza kwa makini Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Mh. Joseph Mbilinyi "Sugu", wakati akizizungumzia changamoto mbali mbali zinaziwakabili wananchi wa jiji hilo, katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika Jijini Mbeya leo Oktoba 18, 2015.

Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akimnadi kwa wananchi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Mh. Joseph Mbilinyi "Sugu", wakati wa Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika Jijini Mbeya leo Oktoba 18, 2015.

Waziri Mkuu wa zamani, Mh. Fredrick Sumaye, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Mbeya katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni za Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe, Jijini Mbeya leo Oktoba 18, 2015.

Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mh. Freeman Mbowe akiwahutubia wananchi wa Jiji la Mbeya waliofurika kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe, wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, leo Oktoba 18, 2015.

Mwanasiasa Mkongwe hapa nchini, Mzee Kingunge ngomale akiwasalimia wananchi wa Jiji Mbeya.










PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO