Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwaambia wananchi wa Karatu katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Bwawani,kuwa mmoja wa viongozi wa upinzani anayempenda kwa dhati, ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt Wilbrod Slaa,amesema kuwa ni kiongozi imara asiyependa kuyumbishwa na kwamba ni kiongozi mwenye msimamo thabiti na mapenzi makubwa na nchi yake Tanzania.PICHA NA MICHUZI JR-KARATU
Umati wa Washabiki na wafuasi wa CCM waliokusanyika katika uwanja wa Bwawani jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni jioni ya leo mjini Karatu,wakishangilia mara baada kumsikiliza sera zake wakati akijinadi na kuomba ridhaa ya kuiongoza nchi katika kipindi cha awamu ya tano kwa nafasi ya Urais.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwanadi wagombea Viti vya Udiwani mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Karatu jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Bwawani mjini humo mkoani Arusha.
Wabunge wa viti maalum wanaowakilisha wanawake watarajiwa kutoka CCM kutoka mkoa wa Arusha, kushoto ni Catherine Magige na Violet Mfuko.
Mgombea Uubunge jimbo la Karatu Dk.Wilbald Slaa Lorri akimuombea kura Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli pamoja na yeye mbele ya wakazi wa mji wa Karatu jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni,kulia kwake ni Wabunge watarajiwa viti maalum wanaowakilisha wanawake mkoa wa Arusha, kushoto ni Catherine Magige na Violet Mfuko wakishangilia.
Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli pichani kushoto akiungana na wasanii Chege na Temba kucheza muziki wakati wa mkutano wa kampeni mjini Karatu, mkoani Arusha.
Mgombea urais wa Tganzania kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni mjini Mbulu, mkoani Manyara jioni ya leo
Dkt. Magufuli akisisitiza jambo mbele ya maelfu ya wananchi wa Mbulu jijini jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni.
Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akiwanadi wagombea ubunge na madiwani mbele ya wakazi wa mji wa Mbulu kwenye mkutano wa kampeni jioni ya leo.
Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi katika Mji wa Haydom, wilayani Mbulu, Manyara ambapo aliwataka wananchi kutowachagua wagombea wanaotoa rushwa kwani wakikubali wanaweza wakawauza wao na Tanzania kwa ujumla
Wananchi wa mji wa Haydom wakimshangilia Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akimwaga sera zake za kujinadi na kuwaomba kura za ndio ifika Oktoba 25 kwenye uchaguzi utakaofanyika mwaka huu kupitia ngazi ya Urais,Ubunge na Udiwani.
Wakazi wa Haydom wakifuatila hotuba ya Dk Magufuli alipokuwa akiwahutubia kwenye mkutano wa kampeni mapema leo mchana mjini humo.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Mbulu Vijijini, Fratei Masay mjini Haydom leo.
Washabiki na wafuasi wa CCM wakiwa na bango lao la ujumbe maridhawa kabisa.
Washabiki na wafuasi wa CCM wakishangilia ujio wa Dkt Magufuli na kuwahutubia kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa Bwawani mjini Karatu,mkoa wa Arusha.
0 maoni:
Post a Comment