By Louis Kolumbia, Mwananchi Digital
Mgombea Ubunge kupitia ACT-Wazalendo Jimbo la Arusha Mjini amafariki dunia katika hospitali ya Kilimanjaro Christian Medical Center (KCMC) usiku wa kuamkia leo .
Makamu mwenyekiti wa ACT-Wazalendo , Shaaban Mambo amezungumza na Mwananchi Digital kwa amepokea simu kutoka kwa mtoto wa marehemu mapema leo asubuhi akimueleza kuwa baba yao amefariki.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa Bw Mallah alijisikia kuumwa siku ya Jumanne Tuesday mara baada ya mkutano wa kampeni za mgombea Urais wa chama hicho Anna Mghwira maeneo ya Ngaramtoni. Akapelekwa hospitali ya St. Thomas Hospital iliyopo Jijini Arusha ambao alikuwa akitibiwa hadi jana alipohamishiwa KCMC kwa matibabu zaidi.
Mipango ya mazishi inaendelea na taarifa itatolewa baada ya kikao cha familia.
Kwa mujibu wa Bw. Mambo, Mallah, aliyekuwa akiongoza Kamati ya fedha ya chama hicho, alikuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa ACT Wazalendo na kwamba chama kimempoteza mtu muhimu sana.
Mwaka 2010, alishinda kiti cha Udiwani Kata ya Kimandolu Ward kupitia CHADEMA. mapema mwaka 2011, Mallah na madiwani wengine watatu wa CHADEMA (John Bayo (Elerai), Reuben Ngowi (Themi) na Charles Mpanda (Kaloleni) walivuliwa uanachama wao katika mgogoro baina ya CCM na Chadema kuhusiana na kilichodaiwa kuwa uchaguzi batili wa meya wa Jiji.
Baadae Bw Mallah akajiunga na ACT-Wazalendo ambapo alipata nafasi ya kuwakilisha chama hicho katika kinyang’anyiro cha Ubunge Arusha Mjini katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe Oktoba 25 mwaka huu, na kupambana na Mbunge anayemaliza muda wake MP Godbless Lema (Chadema). Mshindani mwingine wa Karibu kwa lema ni Bw Philemon Mollel (CCM).
SOURCE: THE CITIZEN
BLOGU HII INAWAPA POLE WAFIWA WOTE HASA, FAMILIA NA CHAMA CHAKE NA MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA. AMINA!
0 maoni:
Post a Comment