Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MWIGULU NCHEMBA AKIOMBA KURA MKOA WA SIMIYU

 

Mwigulu Nchemba akiondoka Jimbo la Maswa Mashariki kumnadi Ndg.Nyongo mbunge mtarajiwa wa Chama cha Mapinduzi.

“CCM mambo yapo Poaaaa!!!”

Mwigulu Nchemba akiwasili eneo la Mkutano akiwa na Mbunge wa Jimbo la Kisesa Ndg.Mpina.

Mbunge mtarajiwa wa Jimbo la Kisesa akizungumza na Wananchi wake kuhusu Moja ya ahadi ya Magufuli ya ujenzi wa Reli ya kisasa itakayopita Kisesa kwenda kanda ya Ziwa kwaajili ya kunufaisha wakulima wa Pamba n.k

“CCM ni Nambari 1″

Mwigulu Nchemba akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Meatu Ndg.Salum Khamis Salum “Jambo”.

Haijalishi wakae Wapi,Wananchi waliamua kupanda Juu ya Miti ilikusikiliza Ujumbe wa Mwigulu Nchemba kwa wanameatu kuelekea Uchaguzi wa Rais,Mbunge na Diwani.Mwigulu amewaomba kumchagua Magufuli mtu wa kazi iliaweze kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Maendeleo ya CCM iliyoweka bayana Ujenzi wa Barabara ya Meatu hadi Singida ilikufungua njia za Uchumi,Pia kwa Kipindi ambacho Meatu ilikuwa Upinzani,Shughuli za Maendeleo zilisimama hapo jimboni.

Hisia za Mwananchi katika maandishi “Magufuli Chaguo la Mungu”.

MwanaCCM akionesha kipeperushi cha Magufuli na Mama Samia Suluhu kuwa ndio Uongozi unaokwenda Kuchaguliwa na Watanzania.

Wananchi wapotayari kuchagua CCM kwa nafasi zote tatu(Udiwani,Ubunge na Urais).

Wanameatu wakifuatilia Mkutano wa kampeni wa Chama cha Mapinduzi kwa Umakini.

“Hakuna wilaya au Mkoa ndani ya Tanzania hii,ambayo Magufuli hajaacha alama ya Ujenzi wa Barabara,Ameunganisha Mikoa kwa mikoa na Wilaya zinaendelea Kuunganishwa,Magufuli hajawahi kushindwa kufanya kazi kwenye wizara yoyote ile.Hivyo tumchague atufanyie kazi Nchi nzima”Mwigulu.

Wananchi wa Meatu wakionesha Utayari wao wa Kuichagua CCM kwenye Uchaguzi Mkuu ujap October 25.

Mwigulu Nchemba akiagana na Wananchi wa Meatu Mjini mara baada ya Mkutano wa hadhara wa kampeni wa Chama cha Mapinduzi.

Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa kata ya Lalago Jimbo la Maswa hii leo wakati wa kuomba kura za Urais,Ubunge na Udiwani kwa Chama cha Mapinduzi.

WanaCCM wakielekea kwenye eneo la Mkutano Jimbo la Meatu.

Mwigulu Nchemba akisalimiana na Mbunge mtarajiwa wa Jimbo la Itilima Ndg.Njalu Silanga jioni ya leo alipofika kuomba kura za Urais,Ubunge na udiwani.

Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Itilima hii.

Wanaitilima wakionesha Kuunga Mkono Kuichagua CCM kwenye Uchaguzi Ujao.

Picha na Sanga Festo Jr.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO