Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mama Samia Aanza Ziara ya Kampeni Mkoani Mwanza, Ahutubia Majimbo Manne LeoPichani juu ni mgombea mwenza wa nafasi ya urais Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi baada ya kusimamishwa barabarani katika Jimbo la Sumve alipokuwa akipita kuelekea Wilaya ya Magu katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kata ya Kisesa Jimbo la Magu.
Baadhi ya wananchi na wanaCCM wa Kata ya Ngudu Jimbo la Kwimba wakiwa katika mkutano wa hadhara wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Mama Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) leo mkoani Mwanza.
Baadhi ya wananchi na wanaCCM wa Kata ya Ngudu Jimbo la Kwimba wakiwa katika mkutano wa hadhara wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Mama Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) leo mkoani Mwanza.
Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Mama Samia Suluhu Hassan (mwenye ushungi) akisalimiana na baadhi ya viongozi na wanaCCM mara baada ya kuwasili Kata ya Ngudu Jimbo la Kwimba kuhutubia mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM uliofanyika leo mkoani Mwanza.
Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Mama Samia Suluhu Hassan (wa kwanza kushoto) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Kata ya Ngudu Jimbo la Kwimba kuhutubia mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM uliofanyika leo mkoani Mwanza. Kulia ni mgombea ubunge wa Jimbo la Kwimba, Mansoor Shanif Hirani.
Mkutano wa hadhara ukiendelea Jimbo la Kwimba
Baadhi ya wanaCCM na makada wa Chama Cha Mapinduzi wakiwa na mabango yenye jumbe anuai kwa mgombea mwenza kwenye mkutano wa hadhara Mji mdogo wa Ngudu.
Msanii Snura Majanga akiimba na kucheza baadhi ya nyimbo zake kuwaburudisha wananchi waliokusanyika katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Mama Samia Suluhu Hassan ulofanyika Jimbo la Kwimba leo mkoani Mwanza.
Sehemu ya wananchi na wanaCCM wa Kata ya Ngudu Jimbo la Kwimba wakiwa katika mkutano wa hadhara wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Mama Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) leo mkoani Mwanza.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza, Antony Diallo akizungumza na wanaCCM na wananchi katika mkutano wa hadhara wa  mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Mama Samia Suluhu Hassan ulofanyika Kata ya Ngudu Jimbo la Kwimba leo mkoani Mwanza.
Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza na baadhi ya wananchi na wanaCCM wa Kata ya Ngudu Jimbo la Kwimba katika mkutano wa hadhara wa kampeni wa ulofanyika leo mkoani Mwanza.
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM Taifa, Anjela Kiziga (kushoto) akijadiliana jambo na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu (kulia) katika moja ya mikutano ya hadhara ya mgombea mwenza wa CCM iliofanyika leo katika Majimbo ya Misungwi, Kwimba, Sumve na Jimbo la Magu.
Sehemu ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa nafasi ya urais Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza baada ya kusimamishwa barabarani katika Jimbo la Sumve alipokuwa akipita kuelekea Wilaya ya Magu katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kata ya Kisesa Jimbo la Magu.
Baadhi ya Wananchi wa Kata ya Kisesa wakishangilia pembezoni mwa barabara kumpokea mgombea mwenza wa nafasi ya urais Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mama Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) alipowasili kufanya mkutano wa hadhara leo. 
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu akizungumza na wananchi na wanaCCM wa Kata ya Kisesa katika mkutano wa hadhara wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Mama Samia Suluhu Hassan ulofanyika leo mkoani Mwanza.


Moja ya kikundi sanaa (kwaya) kikiwaburudisha wananchi na wanaCCM wa Kata ya Kisesa katika mkutano wa hadhara wa kampeni za mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Mama Samia Suluhu Hassan.
Baadhi ya wanaCCM na makada wa Chama Cha Mapinduzi wakiwa na mabango yenye jumbe anuai kwa mgombea mwenza kwenye mkutano wa hadhara Kata ya Kisesa Jimbo la Magu, Mkoani Mwanza.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO