Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

SIASA HAIPASWI KULETA UADUI: WAGOMBEA WA CCM NA CHADEMA WAKUTANA MITAA YA JIJI LA ARUSHA NA KUISHIA KUTANIANA KWA FURAHA NA AMANI

ccm na cdm arusha2

ccm na cdm arusha

ccm na cdm arusha1

ccm na cdm arusha3

ccm na cdm arusha4

ccm na cdm arusha5 

Pichani juu ni baadhi ya matukio ya kufurahisha mchana wa leo baada ya baadhi ya wagombea wa vyama viwili vinavyoshindana kwelikweli katika siasa za mji huu wa Arusha, CHADEMA wanaotaka kuhakikisha wanachukua miliki ya Mji kabisa na CCM wanaopambana kuhakikisha wanarudisha heshima ya chama chao jijini hapa.

Wagombea hao na wapambe wao walikutana katika mitaa ya Jiji katika harakati za kampeni kwa kila chama na kuanza kutaniana na kutambiana kushinda. Hii ni tofauti na inavyodhaniwa na baadhi ya watu ambao wanauelewa mdogo wa masuala ya siasa kwamba upinzania wa siasa ni uadui.

Blogu hii inapongeza sana ukomavu wa kisiasa uliooneshwa na wafuasi wa vyama vyote viwili na unahimiza ukomavu huo uenziwe na uendelee mpaka wakati wa uchaguzi oktoba 25 mwaka huu na kila mmoja awe tayari kukubaliana na wananchi watakavyoamua.

Picha na Martin Munis wa UVCCM Arusha.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO