Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MKUTANO WA LOWASSA MOSHI MJINI; AAHIDI NEEMA KWA WAKULIMA WA ZAO LA KAHAWA KILIMANJARO

Kada mkongwe wa Chama cha Mapinduzi,aliyejiengua hivi karibuni ,Kingunge Ngombalemwiru akisalimia wakati wa mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea Urais kupitia Chadema na Vyama vinavyounda Umoja wa katiba ya wananchi UKAWA uliofanyika katika viwanja vya mashujaa mjini Moshi.Picha zote na Dixon Busagaga wa Busagaga's Orijino Blog.
Kada mkongwe wa Chama cha Mapinduzi,aliyejiengua hivi karibuni ,Kingunge Ngombalemwiru akimkaribisha mgombea Urais kupitia Chadema na Vyama vinavyounda Umoja wa katiba ya wananchi UKAWA ,Edward Lowasa kuzungumza na wakazi wa mji wa Moshi katika viwanja vya Mashujaa mjini Moshi.
Mgombea Urais kupitia Chadema chini ya mwavuli wa vyama vinavyounda Umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) ,Edward Lowasa akizungumza na maelfu ya wakazi wa mji wa Moshi na Vitongoji vyake waliofika kumsikiliza katika mkutano uliofanyika viwanja vya Mashujaa mjini hapa.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ,(Chadema) taifa ,Freeman Mbowe akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mashujaa Mjini Moshi.

Maelefu ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wa kampeni wa mgombea Urais kutia Chadema kwa mwavuli wa vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA,wakionesha ishara ya mabadiliko.
Mwenyekiti mwenza wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi,UKAWA,James Mbatia akizungumza katika mkutano wa kampeni wa kumnadi mgombea Urais ,Edward Lowasa uliofanyika katika uwanja wa Mashujaa mjini Moshi.

Mwenyekiti Mwenza wa vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA,James Mbatia akiwa amemnyanyua mkono na kumuombea kura mgombea Ubunge katika jimbo la Moshi mjini ,Jafary Michael
Mgombea Ubunge katika jimbo la Moshi mjini ,Jafary Michael (Chadema) akizungumza na maelefu ya wananchi waliofurika katika uwanja wa Mashujaa mjini Moshi katika mkutan wa kampeni wa kumnadi mgombea Urais kupitia UKAWA,Edward Lowasa.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO