Katibu wa Mbunge wa Arusha Mjini, Bw Methew Kishili (pichani) kutoka Arumeru Mashariki amejitokeza kuwanina nafasi ya kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana Chadema Taifa (BAVICHA) katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Septemba 10 mwaka huu katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam. Ufuatao ni wasifu wake kama ambavyo Blog hii imeupata.
Nakusalimu Kamanda!
Jina langu ni Mathew Kishili, kijana Mtanzania wa kuzaliwa, mpambanaji wa Chadema na kwa sasa Mgombea nafasi ya Katibu wa BAVICHA Taifa.
Kwanini Nafaa kuwa KATIBU WA BAVICHA!? Zifuatazo ni Dondoo za Wasifu Wangu Kielimu, Kijamii na Kisiasa.
Tarehe ya kuzaliwa kwangu ni 29/07/1984
Nina Elimu ya Shahada ya kwanza ya Maendeleo ya Jamii na Usimamizi wa Miradi kutoka Chuo cha CDTI-Tengeru, Arusha.
Nilijiunga na chama cha Demokrasia na Maendeleo mwaka 2009, tangia wakati huo nimekuwa mtiifu kwa chama nikikua kiuongozi ndani ya chama.
Uongozi Ndani ya Chama
Nimekuwa Kaimu Katibu wa Chadema Wilaya Arumeru Mashariki kuanzia 2012-2014
Nimekuwa Mwenyekiti wa Vijana (BAVICHA) Arumeru Mashariki kuanzia mwaka 2010 hadi sasa
Nimekuwa Katibu wa Kata wa Chadema Kata ya Nkoaranga
Nimekuwa Katibu wa Tawi la Chadema Chuo Cha CDTI-Tengeru wakati wote nikiwa mwanafunzi.
Nimekuwa Meneja kampeni za Chadema kwa Chaguzi za kuunda Mamlaka ya Mji Mdogo USA River ambapo Chadema ilishinda Mitaa 6 kati ya 9 iliyokuwa inashindaniwa.
Uongozi nje ya Chama
Nimekuwa Katbu wa Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema kuanzia mwaka 2013 hadi sasa.
Nimekuwa Waziri wa Mikopo Chuo cha CDTI-Tengeru mwaka 2010/11.
Nimekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Miradi ya Vijana KKKT Usharika wa Nkoaranga
Malengo yangu na BAVICHA Mpya!!
Malengo yangu ndani Baraza la Vijana Taifa (BAVICHA) ni kuhakikisha Baraza linajitegemea katika uendeshaji wa operation zake na kupunguza utegemezi kwa chama kwa kiwango kikubwa kwa kuhakikisha Baraza la Vijana linakuwa na rasilimali zake zenyewe kama ardhi angalau kila Wilaya.
Kujengea vijana uwezo hasa nyanja za siasa, ujasiriamali, elimu ya sheria nk
Kuhamasisha Vijana kushiriki chaguzi kwa kupiga kura na kupigiwa kura.
Kutumia uzoefu wangu wa kiuongozi ndani na nje ya chama kuwaunganisha vijana nchini kuwa na sauti moja katika kupigania mustakabali wa taifa letu na chama chetu kwa ujumla.
0 maoni:
Post a Comment