Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Watuhumiwa wa mabomu Arusha wapandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka ya mauaji

 

Watuhumiwa wapatao 19 wanaotuhumiwa kwa milipuko ya mabomu mkoani Arusha leo wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Arusha na kusiomewa mashtaka mbalimbali yanayo wakabili yakiwemo ya mauaji.Watuhumiwa hao ambao wameunganishwa na wenzao zaidi ya 20 waliokwishafikishwa kwenye mahakama hiyo kwa tuhuma hizo wamefikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa polisi ambao haujawahi kuonekana katika siku za hivi karibuni.

Gari ya polisi iliyowabeba watuhumiwa hao


Tofauti na ilivyokuwa hapo awali ulinzi katika mahakama hiyo uliiimarishwa kwa kiasi kikubwa kuanzia mapema alifajiri ambapo watu wote waliokuwa wanaingia kwenye lango la mahakama hiyo walikaguliwa na vifaa maalumu utaratibu ambao ulifuatwa na watu wote bila kujali nyadhifa zao wakiwemo watendaji wa mahakama hiyo.


Baada ya kufikishwa mahakamani hapo mbele ya hakimu Devota Msofe aliyekuwa anasaidiwa na waendeshamashtaka Agustino Kombe, Felexs Kwetukia na Maselina Mwamunyange washtakiwa walisomewa mashtaka yanayowakabili kwa makundi, jinsi wanavyodaiwa kuhusika na madhara yaliyosababishwa na makosa hayo.Miongoni mwa mashataka waliyosomewa ambayo kila mmoja alihusishwa kwa namna moja ama nyingine huku baadhi yao wakijikuta wakitajwa karibu kwenye makosa yote ni pamoja na shtaka la mauaji, kujihusisha na vitendo vya kigaidi, kukusanya silaha yakiwemo mabomu, kuyasarisha na kisha kuyatumia kuua na pia kufadhili vitendo hivyo kwa kutoa fedha na ushirikiano wa kuvitelekeza.


Mashtaka mengine ni pamoja na kushawishi na kuhamasisha vijana kujiunga na vikundi vya ugaidi, kuhifadhi dhana na silaha za kwa lengo la kufanya ugaidi na kuzitumia kutekeleza vitendo hivyo.


Kesi ya watuhumiwa hao ambao wote wanahusishwa na matukio yote ya milipuko ya mabomu na kuwamwagia viongozi wa dini tindikali vilivyowahi kutokea mkoani Arusha itatajwa tena tarehe 15.08/2014 na washtakiwa wote wamerudishwa rumande ambapo kwa mujibu wa sheria kesi yao haina dhamana.

 

STORI NA PICHA: MATUKIO NA VIJANA .COM

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO